Marioo
Marioo (jina lake halisi ni Omary Mwanga; alizaliwa mwaka 1995, Temeke, Dar es Salaam, Tanzania) ni mwimbaji wa Bongo Flava, mtunzi na mtayarishajipia wa nyimbo. Alilelewa kijijini kwa bibi yake Kibiti, mkoa wa Pwani, na huko ndiko alikokulia, akiwa ni mtoto wa kabila la Wandengereko.
Marioo alianza safari yake ya muziki kama mtunzi wa nyimbo, ambapo alitunga nyimbo kama Wasikudanganye, aliyoimba mwanamuziki wa Tanzania, Nandy The African Princess. Aidha, aliandika wimbo wa Unaniweza, alioimba Jux, na yeye ndiye mmiliki wa wimbo maarufu Beer Tamu, uliohushinda tuzo za TMA kama wimbo bora wa mwaka 2021 na 2022.
Wimbo wake wa kwanza katika safari ya muziki ni Dar Kugumu, alioutoa mwaka 2017. Baada ya hapo, alijizolea umaarufu kwa kutoa nyimbo zingine kama Inatosha, Unanionea, AYA, Raha, Chibonge, Salio, Lonely, Unanichekesha, Mama Aminah, Hakuna Matata, na Beer Tamu.
Pia, Marioo amefanikiwa kufanya kolabo na wasanii kutoka nchi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na wasanii kutoka Afrika Kusini. Amejizolea mashabiki wengi kutokana na sauti yake laini na uwezo wake wa kuandika nyimbo zenye ujumbe mzito na mguso wa kihisia. Mbali na muziki, Marioo pia ameonyesha nia ya kuwekeza katika biashara na kusaidia jamii kupitia miradi mbalimbali ya kijamii. Aidha, Marioo amefanikiwa kushinda tuzo ya Msanii Bora wa Mwaka 2024.
Tuzo
hariri- Mwanamuziki bora wa kiume wa mwaka TMA 2022
- Nyimbo bora ya mwaka "bia tamu"
- Mtunzi bora wa mwaka 2024
Tanbihi
haririMakala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Marioo kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |