Nandy
Nandy (amezaliwa Kilimanjaro, Tanzania, 9 Novemba, 1992) ni mwimbaji na mtunzi wa nyimbo kutoka nchini Tanzania.
Nandy | |
---|---|
Nandy juu ya jukwaa la Tamasha la Fiesta mjini Dodoma, Tanzania, 2017 | |
Taarifa za awali | |
Jina la kuzaliwa | Faustina Charles Mfinanga |
Amezaliwa | Mawenzi, Moshi, Tanzania | Novemba 9, 1992 (age 32)
Kazi yake | |
Miaka ya kazi | 2010–hadi sasa |
Mwaka wa 2017 alishinda tuzo ya All Africa Music Awards katika kundi la wasanii bora wa kike kutoka Afrika Mashariki.[1][2]
Maisha ya awali
haririNandy alizaliwana Mary Charles, fundi kushona, na Charles Mfinanga, ambaye ni fundi makenika. Jina la Nandy ni kifupi cha jina lake halisi Nandera. Alianza kutumbuiza akiwa na umri mdogo kabisa. Akiwa na miaka mitano, alikuwa mwanachama hai wa kwaya ya mafunzo ya Jumapili ya Kanisa la KKKT huko Moshi. Alimaliza elimu ya msingi katika shule ya msingi ya Mawenzi, baadaye kajiunga Lomwe High School ambako huko alikuwa mwana-kwaya mkuu katika shule hiyo. Baada ya kumaliza elimu ya juu alijiunga na Chuo cha Biashara (CBE), Dar es Salaam, Tanzania.
Kazi
haririTanzania House of Talent
haririKazi yake ilianza kujulikana baada ya rafiki yake kumtambulisha kwa Ruge Mutahaba, Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania House of Talent (THT). Hapa ndipo alipokutana na Ema the Boy, ambaye ndiye aliyekuja kumtayarishia kibao chake maarufu cha Nagusagusa.Wimbo ulikuja kutamba mno wiki tu tangu kutolewa kwake.
Mwanzoni mwa mwaka wa 2016 alishiriki kwenye mashindano ya kuimba yaliyoandaliwa na Tecno. Shindano lilishirikisha washiriki wengine kutoka nchi kibao za Afrika na kipindi cha fainali kilichofanyika huko Lagos, Nigeria, Nandy aliibuka kama mshindi wa pili. Shindano hili lilimkuza kimuziki, hasa katika suala zima la utumbuizaji jukwaani, alipata maarifa ya muhimu kutoka kwa magwiji wa muziki kama vile akina M.I Abaga, Yemi Alade na Bien wa Sauti Sol.[3][4]
Mwaka wa 2017 alitoa kibao cha One Day ambacho kilisukuma kazi yake na hatimaye kumpa nafasi kadhaa zilizomfanya kushiriki kwenye Coke Studio Africa 2017 na mwaka huohuo akaja kuchaguliwa kwenye tuzo za All Africa Music Awards katika kundi la wanamuziki bora wa kike kutoka Afrika Mashariki na kuibuka mshindi na akatoa kibao kiitwacho kivuruge na hivi sasa anatamba na wimbo wake ambao amefanyakazi yeye na willy paul ambao jina lake ni hallelujjah[5][6][7][8][9]
Mbali na muziki, yeye ni mpenda mitindo na ndiye mmiliki wa Prints by Nandy Africa. Yeye pia ni balozi wa UNICEF, mwanamitindo wa nguo za harusi za kina dada na miliki wa Make up by Nandy.[10]
Albamu
hariri- African Princess (2018)[11]
Singo
hariri- I'm Confident (2013)
- Nagusa gusa (2017)
- One Day (2017)[12]
- Wasikudanye (2017)
- Kivuruge (2017)[13]
- Ninogeshe (2018)[14]
Tuzo na chaguzi
haririMwaka | Shere ya Tuzo | Tuzo | Mpokeaji | Tokeo |
---|---|---|---|---|
2017 | All Africa Music Awards[1][2] | Msanii Bora wa Kike Afrika Mashariki | Nandy | Ameshinda |
2018 | AMI Awards Afrika[15] | Msanii Bora Chipukizi | Nandy | Kigezo:Pending |
Marejeo
hariri- ↑ 1.0 1.1 "AFRIMA 2017: Full list of winners", Music In Africa, 2017-11-13. (en)
- ↑ 2.0 2.1 Azaniapost. "Bongo Flava: Ali Kiba, Nandy win awards at AFRIMA in Nigeria", Azaniapost. Retrieved on 2018-07-30. (tr) Archived from the original on 2018-07-29.
- ↑ "29-year-old wins $25K, recording deal", pulse.ng. Retrieved on 4 May 2018. (en-us)
- ↑ "Tanzania: Heartbreak for Tanzania's Nandy in Lagos", allafrica.com. Retrieved on 4 May 2018. (en-us)
- ↑ "MEET THE AFRICAN PRINCESS". coca-cola.co.ke. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-08-14. Iliwekwa mnamo 4 Mei 2018.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Nandy: Mane Fitsum (Cover) - Coke Studio Africa". coca-colacompany.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-06-27. Iliwekwa mnamo 4 Mei 2018.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Aslay – Subalkheri Mpenzi Ft Nandy". celebvibestar.co.ke. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-06-27. Iliwekwa mnamo 4 Mei 2018.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Coke Studio Africa 2017 Officially Launches In Ethiopia". ethiosports.com. Iliwekwa mnamo 4 Mei 2018.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Nandy and AliKiba shine at Afrima". thecitizen.co.tz. Iliwekwa mnamo 4 Mei 2018.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ https://mdundo.com/news/31026
- ↑ "The African Princess | Mistari Yetu: Albamu ya Nandy The African Princess". Mistari Yetu (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-10-31. Iliwekwa mnamo 2019-09-10.
- ↑ "Nandy – One Day". notjustok.com. Iliwekwa mnamo 4 Mei 2018.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "New Music: Nandy – Kivuruge". uplandradiofm.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-05-05. Iliwekwa mnamo 4 Mei 2018.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Nandy – Ninogeshe". tooxclusive.com.ng. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-06-27. Iliwekwa mnamo 4 Mei 2018.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "AMI Awards Afrika 2018 full nominee list". whatshappeningmagazineug.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-07-31. Iliwekwa mnamo 4 Mei 2018.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Viungo vya Nje
hariri- Nandy: Youtube
- Nandy: MistariYetu Archived 23 Oktoba 2019 at the Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Nandy kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |