Mary Rusimbi

mwanaharakati, mtafiti na mshauri wa masuala ya jinsia na maendeleo

Mary Rusimbi ni mwanamke Mtanzania ambaye ni mwanaharakati, mtafiti na mshauri wa masuala ya jinsia na maendeleo.

Mary Rusimbi
Amezaliwa
Tanzania
Nchi Tanzania
Kazi yake Mwanaharakati mtafiti na mshauri wa masuala ya jinsia na maendeleo

Alipata shahada yake ya kwanza ya elimu ya watu wazima katika chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Alipata pia cheti cha elimu ya maendeleo ya jinsia London nchini Uingereza.

Amefanya kazi na balozi mbalimbali kama mtaalamu wa jinsia ukiwemo ubalozi wa Canada na Ubalozi wa Ujerumani.

Mwaka 1983 alikwenda nchini New Zealand kwa masomo zaidi na kupata stashahada yake katika elimu ya jamii.[1].

Mafanikio yake hariri

Kama mwanaharakati mwanamke amefanikiwa kuwa sehemu na mwanzilishi mshiriki wa Tanzania Gender Networking Program (TGNP)[2]. Pia ni mwanachama wa Foundation for Civil Society ambayo ni jumuiya inayojitegemea isiyo ya faida inayoziwezesha jumuiya nyingine kuwasaidia wananchi katika mchakato wa maendeleo na utawala bora.[3].

Marejeo hariri

  1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-08-28. Iliwekwa mnamo 2018-09-08. 
  2. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-08-28. Iliwekwa mnamo 2018-09-08. 
  3. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-09-11. Iliwekwa mnamo 2018-09-08. 
  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mary Rusimbi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.