Matamvua ya samaki (pia: mashavu ya samaki; kwa Kiingereza: gills) ni viungo kwenye mwili wa samaki na wanyama wengine wanaoishi kwenye maji vinavyowawezesha kupumua, yaani kupeleka oksijeni iliyomo mwenye maji kuingia katika damu. Yanatoa pia hewa iliyotumiwa ya dioksidi kabonia kutoka damu na kuiacha kwenye maji. Kwa hiyo matamvua ya viumbehai wa majini hutekeleza kazi inayolingana na mapafu ya wanyama wa nchi kavu.

Matamvua ya kamongo yanaonekana kwa sababu alizaliwa bila mfuniko unaoyafunika kwa kawaida.
Matamvua ya jodari.
Matamvua ya kiluwiluwi za salamanda.

Matamvua huhitaji kwa kazi hiyo uso mkubwa ambamo mishipa ya damu katika ngozi yake huitishwa na maji yenye oksijeni. Kwa hiyo umbo lake linaweza kufanana na unyoya.

Samaki huwa na matamvua kando ya kichwa. Ndubwi (viluwiluwi) wa amfibia mara nyingi huwa na matamvua yanayotoka nje ya mwili.

Wanyama wadogo sana wa majini hawahitaji matamvua kwa sababu kwao upumuo hutokea moja kwa moja kupitia ngozi ya mwili.

Viungo vya nje hariri

 
Simple English Wiktionary
Wikamusi ya Kiswahili ina maelezo na tafsiri ya maana ya neno:
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Matamvua (samaki) kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.