Tawimto
Tawimto[1] (kwa Kiingereza: tributary) ni mto unaoishia katika mto mwingine ambao kwa kawaida ni mkubwa zaidi.
Kwa kawaida maji ya eneo fulani hutiririka chini na kuwa vijito na mito hadi kuishia katika mto mkuu unaobeba maji yote hadi baharini, ziwa kubwa, madimbwi au wakati mwingine katika sehemu ya jangwa yanapopotea. Mto unaofikia mwisho hutazamwa kuwa mto mkuu wa beseni, na mingine yote ni matawimto yake, ama moja kwa moja au kupitia tawimto lingine.
Wataalamu wakiorodhesha mito yote ya beseni la mto fulani hutumia hasa taratibu mbili tofauti za kuorodhesha mito hii:
Matawimto huorodheshwa kuwa ya kushoto au kulia. Hapo msimamo daima hufuata mwelekeo wa maji kutoka chanzo kwenda mdomoni. Kwa mfano pala ambako mto Ruvuma ni mpaka kati ya Tanzania na Msumbiji ukielekea Bahari Hindi, mito yote inayoingia Ruvuma kutoka upande wa Msumbiji ni matawimto ya kulia, mito yote inayoingia kutoka upande wa Tanzania ni matawimto ya kushoto.
Marejeo
hariri- ↑ Neno hili "tawimto" haijatumiwa sana na waandishi na wasemaji wa Kiswahili, ni kati ya istilahi za sayansi zilizopendekezwa na kamusi ya KAST, uk.306.
Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.
|