Muungano wa kifalme

(Elekezwa kutoka Maungano ya kifalme)

Muungano wa kifalme ni hali ya kisiasa na ya kisheria ambako nchi mbili au zaidi zinachanga mtu yuleyule kama mfalme wao au mkuu wa dola.

Nchi zote hizo zinaendelea kuwa madola ya pekee lakini mfalme ni yeye yule.

Muungano wa aina hiyo hupatikana katika utaratibu wa utawala wa kifalme lakini haipatikani katika utaratibu wa kijamhuri.

Wakati wa sasa

hariri

Mifano ya siku hizi ni hasa Jumuiya ya Madola. Nchi nyingi za jumuiya hiyo zinamtambua mfalme Charles III wa Uingereza kama mkuu wa dola kufuatana na katiba ya nchi. Mfalme anamteua gavana mkuu kama mwakilishi wake nchini. Katika utaratibu huo nchi hizo zitamtambua pia mfalme au malkia atakayemfuata Charles III kufuatana na sheria za Uingereza kuwa mkuu mpya wa nchi yao.

Nchi ndogo ya Andorra kati ya Ufaransa na Hispania ni mfano wa pekee ambako rais wa jamhuri anakuwa mkuu wa dola wa nchi nyingine. Tangu mwaka 1607 nafasi ya mkuu wa dola wa Andorra hushirikishwa kati ya askofu wa Urgel (Hispania) na mfalme wa Ufaransa. Baada ya mapinduzi ya Ufaransa mwaka 1789 rais wa jamhuri alichukua nafasi ya mfalme wa awali.

Mifano ya kihistoria

hariri

Historia ina mifano mingi ya muungano wa kifalme kati ya nchi mbili zilizoendelea na taratibu zao za pekee lakini kumchanga mfalme yeye yule.