Mavanga
Mavanga ni kata ya Wilaya ya Ludewa katika Mkoa wa Njombe, Tanzania. Msimbo wa posta ni 59416.
Kata ya Mavanga | |
Nchi | Tanzania |
---|---|
Mkoa | Njombe |
Wilaya | Ludewa |
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 9,738 |
Kata ya Mavanga ina vijiji viwili ambavyo ni Mavanga na Mbugani.
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 9,738 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 7,651 [2] walioishi humo. Hii ni moja ya kata ambayo idadi ya watu inaongezeka kwa kasi na hivyo kuifanya moja ya miji midogo inayokua kwa kasi katika Wilaya ya Ludewa.
Katika kata ya Mavanga wakazi wake hujishughulisha na kilimo cha mazao mbalimbali kama maharage, mahindi, viazi vitamu, ufuta, ndizi, mihogo, miwa, karanga, njugu mawe, kunde na mengineyo.
Kata ya Mavanga ina shule za msingi tano: nne hutumia Kiswahili na moja hutumia lugha ya kiingereza. Shule hiyo ni Saint Mary Immaculate Primary School iliyopo chini ya Parokia ya Mavanga. Aidha kata ya Mavanga ina Shule ya Sekondari moja.
Mavanga ni moja kati ya kata ambazo zimepata huduma ya umeme wa maji kutokana na mradi wa Umeme wa Maji (Small Scale Hydro electric Power Plant) kwa ufadhili kutoka Duren, Ujerumani, chini ya usimamizi wa Kanisa Katoliki, Jimbo la Njombe.
Marejeo
hariri- ↑ https://www.nbs.go.tz, uk 210
- ↑ "Sensa ya 2012, Njombe - Ludewa DC" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2004-01-02. Iliwekwa mnamo 2017-03-16.
Kata za Wilaya ya Ludewa - Mkoa wa Njombe - Tanzania | ||
---|---|---|
Ibumi | Iwela | Kilondo | Lifuma | Luana | Lubonde | Ludende | Ludewa | Lugarawa | Luilo | Lumbila | Lupanga | Lupingu | Madilu | Madope | Makonde | Manda | Masasi | Mavanga | Mawengi | Milo | Mkongobaki | Mlangali | Mundindi | Nkomang'ombe | Ruhuhu |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Njombe bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Mavanga kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno. |