Wilaya ya Ludewa
Wilaya ya Ludewa ni wilaya mojawapo ya Mkoa wa Njombe.

Katika sensa ya mwaka 2002, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 128,520 [1].
Ludewa iko upande wa kaskazini-mashariki ya Ziwa Nyassa. Makao makuu ni mji wa Ludewa. Wilaya imepakana na wilaya za Njombe na Makete, upande wa mashariki na mkoa wa Ruvuma na upande wa kusini na nchi ya Malawi ng'ambo ya ziwa.
Wenyeji asilia wa Ludewa ni Wapangwa, Wakisi na Wamanda.
Karibu na Lugarawa akiba kubwa ya mtapo wa chuma imetambuliwa kuna mpango wa kuanzisha migodi ya Liganga. Akiba ya madini za chuma ni zaidi ya tani bilioni 1 na hivyo akiba kubwa inayojulikana Afrika. Kuna mradi wa kampuni ya Kichina Sichuan Hongda Group Ltd inayotaka kuzalisha feleji kwa kutumia makaa kutoka akiba ya Mchuchuma karibu na Ziwa Nyasa[2]
Marejeo Edit
- ↑ Sensa ya 2012, Njombe Region
- ↑ [read:https://www.thecitizen.co.tz/news/Liganga--Mchuchuma-iron-ore--coal-deals-for-review/1840340-5416296-psmqlbz/index.html Liganga, Mchuchuma iron ore, coal deals for review], tovuti ya Citizen TZ, tar. 13.01.2020
Kata za Wilaya ya Ludewa - Mkoa wa Njombe - Tanzania | ||
---|---|---|
Ibumi | Iwela | Kilondo | Lifuma | Luana | Ludende | Ludewa | Lugarawa | Luilo | Lumbila | Lupanga | Lupingu | Madilu | Madope | Makonde (Ludewa) | Manda (Ludewa) | Masasi (Ludewa) | Mavanga | Mawengi | Milo | Mkongobaki | Mlangali (Ludewa) | Mundindi | Nkomang'ombe | Ruhuhu |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Njombe bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Wilaya ya Ludewa kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno. |