Mayo (Bumbuli)

(Elekezwa kutoka Mayo)

Mayo ni kata ya Wilaya ya Bumbuli katika Mkoa wa Tanga, Tanzania. Mayo ni sehemu ya tarafa ya Bumbuli. Kijiji cha Mayo kipo kwenye mlima, upande wa mashariki wa mji wa Bumbuli. Kijiji cha Mayo kinapakana na kijiji cha Mgwashi kwa upande wa Kaskasini Mashariki. Vijiji vya Mayo na Mgwashi vinatenganishwa na msitu mkubwa wa Mazumbai.

Kijiji cha Mayo

Watu na uchumi

hariri

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 5,187 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 12,218 waishio humo.

Wakazi wa eneo hili ni hasa Wasambaa na shughuli yao kubwa ni kilimo cha mazao ya chakula na ya biashara. Zao kubwa la biashara kwa wakazi wa kata ya mayo ni majani ya chai. Licha ya zao la ndizi kuwa la chakula, lakini wakazi wa Mayo hulifanya kama zao la biashara pia.

Marejeo

hariri
  Kata za Wilaya ya Bumbuli - Mkoa wa Tanga - Tanzania  

Baga | Bumbuli | Dule "B" | Funta | Kisiwani | Kwemkomole | Mahezangulu | Mamba | Mayo | Mbuzii | Mgwashi | Milingano | Mponde | Nkongoi | Soni | Tamota | Usambara | Vuga


  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Tanga bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mayo (Bumbuli) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.