Mbwawa ni kata ya Kibaha Mjini katika Mkoa wa Pwani, Tanzania yenye postikodi namba 61111 .

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 5,846 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 4,008 [2] walioishi humo.

Kijiji hicho hiki kinapakana na kijiji cha Miswe kwa upande wa kaskazini, Msitu wa hifadhi(forest reserve) kwa upande wa mashariki, Vikuruti kwa upande wa kusini.

Kijiji hiki kimebahatika kuwa na vyanzo vingi vya maji ikiwemo Mto Ruvu unaopatikana upande wa Magharibi ya kijiji, mabwawa (Bwawa la Mbwawa ambalo ni chimbuko la jina la kijiji) na visima vikiweko vya Ving'andi, Kwa Ulaiti, Kwa Kibagaza na Mwa Mbango.

Vitongoji vya kijiji cha Mbwawa ni pamoja na Hekani, Shuleni, Mkoleni, Kitonge,Bomu, Soweto, Madabala, Bangalala, Mzigula etc.

Watu maarufu katika Mbwawa ni pamoja na Sulemani Kisumni, Selemani Fundi Dendego, Iddi Mvumba, Shabani Mgeni, Mbango(marehemu), Ding'anda (Marehemu), Divaza (Marehemu), Ulaiti (Marehemu), Mintanga, Salum Gereza, Waziri Mwinyi mwawila (Digumile), Rajabu Waziri Mwinyi (Bagilo), Hussein Waziri Mwinyi, Mnyimvua Pazi (Marehemu), Juma Upara, Kondo Matambo (marehemu), Shabani Kilenga, Mnyimvua Kilenga.

Walimu waliowahi kufundisha shule ya msingi Mbwawa ni pamoja na Sudi Mweluala, Omari Saidi Msonde(marehemu), Gahu, Willson, Michese (Ms), Chitawala (Mr), Abdallah Makinga (Mr) nk.

Ardhi ya Kijiji cha Mbwawa ni nzuri na yenye rutuba ya asili. Kilimo kikubwa kijijini hapa ni pamoja na mihogo, Ufuta, Mananasi, Minazi, Migomba, maembe na mpunga.

Makabila yanayopatikana kijini mbwawa ni mchanganyiko, ikiwemo Wazaramo, Wakwele, Wazigua, Wangindo, Wamakonde, Wasukuma, Wandengeleko. Asilimia kubwa ikiwa ni Wazaramo.

Kijiji hiki chenye ardhi nzuri iliyo tambarare inayojumuisha milima kiasi, kina bahati ya kuwa na huduma nyingi za msingi ikiwa ni pamoja na zahanati ya serikali, shule ya msingi ya serikali, sekondari ya mission, barabara na usafiri wa uhakika, umeme, maji nk.

Marejeo hariri

  1. https://www.nbs.go.tz
  2. "Sensa ya 2012, Pwani - Kibaha TC". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2004-01-02. Iliwekwa mnamo 2016-06-18. 
  Kata za Wilaya ya Kibaha Mjini - Mkoa wa Pwani - Tanzania  

Kibaha | Kongowe | Mailimoja | Mbwawa | Misugusugu | Mkuza | Msangani | Pangani | Picha ya Ndege | Sofu | Tangini | Tumbi | Visiga | Viziwaziwa

  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Pwani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mbwawa kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.