McKinsey & Company
McKinsey & Company ni kampuni ya kimataifa ya ushauri wa masuala ya usimamizi duniani. Inafanya uchambuzi wa kutathmini maamuzi ya usimamizi katika sekta za umma na za kibinafsi. McKinsey inachapisha jarida la McKinsey Quarterly tangu mwaka wa 1964, inafadhili shirika la utafiti la the McKinsey Global Institute, linachapisha taarifa mbalimbali juu ya mada ya usimamizi, na linaandika vitabu vingi vya juu ya mada ya usimamizi.
Historia
haririMcKinsey & Company ilianzishwa Chicago ikiitwa James O. McKinsey & Company mwaka 1926 na James O. McKinsey, profesa wa uhasibu katika Chuo Kikuu cha Chicago[1] [2]ili kutumia kanuni za uhasibu kwenye mada ya usimamizi.
McKinsey alikufa mwaka wa 1937, na kampuni hiyo ilirekebishwa mara kadhaa; McKinsey ya kisasa ilijitokeza mwaka 1939.
Marvin Bower anachukuliwa kuwa ndiye aliyejenga utamaduni na kanuni za McKinsey katika miaka ya 1930 kulingana na uzoefu wake kama mwanasheria. Kampuni hii ndiyo ilianzisha sera ya "juu au nje", ambapo washauri ambao hawapandishwi cheo wanaombwa kuondoka. McKinsey ilikuwa kampuni ya kwanza ya ushauri kuajiri wahitimu wa hivi karibuni wa chuo, badala ya mameneja wazoefu.
Katika miaka ya 1980 na 1990, kampuni hiyo ilienea kimataifa. Ilikuwa na wafanyakazi 88 mwaka 1951 na 7,700 mwanzoni mwa mwaka 2000. Ushauri wa McKinsey umesaidia kuanzisha kanuni nyingi zinazotumika katika biashara na kuchangia kwa mafanikio na pia kushindwa kwa mengi katika biashara katika zama za kisasa.
Marejeo
hariri- ↑ Walter Kiechel (Desemba 30, 2013). Lords of Strategy: The Secret Intellectual History of the New Corporate World. Harvard Business Press. uk. 55. ISBN 978-1-4221-5731-2.
{{cite book}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ David Snider; Chris Howard (Februari 16, 2010). Money Makers: Inside the New World of Finance and Business. Palgrave Macmillan. uk. 152. ISBN 978-0-230-61401-7.
{{cite book}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Viungo vya nje
hariri- Tovuti rasmi
- Filamu fupi kuhuu historia ya McKinsey & Company
- McKinsey Quarterly Ilihifadhiwa 4 Februari 2012 kwenye Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu McKinsey & Company kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |