Mchezo wa pool (kwa Kiingereza "Pool" au "Billiards") ni mchezo ambao unachezwa na watu wawili au hata zaidi kwa kutumia mipira minane ya rangi pamoja na mpira mmoja mweupe, pia na fimbo ndefu.

Mchezo wa Pool.

Mchezo huchezwa sana katika nchi za Ulaya na Australia, uwanja wake una vitundu au mifuko sita au nane kwa ajili ya kuingizia mpira.

Mchezo wa pool ni kati ya michezo inayopendwa sana na vijana. Pool huwa na bodi yenye vijishimo ambapo vijana hupiga vijipira kwa miti huku lengo lao likiwa kuweka mipira yote kwa vishimo. Kila mchezaji hujaribu kila awezalo kuhakikisha kwamba yeye ndiye atakayerusha mipira mingi zaidi ndani ya vile vijishimo.

Mchezo wa pesa

hariri

Kwa jamii nyingi, mchezo huu wa pool huchezwa katika vilabu, au hata madukani penye vijana wengi na wazee. Wachezaji wengi wa pool hutumia pesa ili kwamba atakayeshinda katika pool anashinda tita la pesa.

Nini kinachohitajika

hariri

Ili uweze kuibuka mshindi wa pool, lazima uwe na jiti zuri (yaani cue stick) ambayo itaweza kurusha mipira kwa urahisi.

Yafaa pia bodi ya pool iwe nzuri yenye kitambaa chororo ili kwamba iwe rahisi kwa mipira kubingirika hadi kwenye vishimo.

Viungo vya Nje

hariri
  Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Mchezo wa pool kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.