Metodi wa Olimpo

(Elekezwa kutoka Methodi wa Olympus)

Metodi wa Olimpo (alifariki mwaka 311 hivi) alikuwa askofu wa Olimpo (Lycia) na mfiadini kutoka Anatolia (leo nchini Uturuki)[1].

Taarifa za kwanza juu yake ziliandikwa na mtakatifu Jeromu[2]

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu na babu wa Kanisa.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 20 Juni[3]

Maandishi

hariri

Metodi aliandika sana na kwa ufasaha kuhusu masuala ya teolojia, akipinga uzushi wa wakati wake na hasa ule wa mafundisho kadhaa ya Origen.

Kwa bahati mbaya, vitabu vyake vimepotea kwa kiasi kikubwa. Kilichotufikia kizima kwa Kigiriki kinahusu ubikira (Symposion e peri hagneias).[4]

Kati ya matoleo ya maandishi yake kuna: Patrologia Graeca, XVIII; Jahn, S. Methodii opera et S. Methodius platonizans (Halle, 1865); Bonwetsch, Methodius von Olympus: I, Schriften (Leipzig, 1891).

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  1. https://www.santiebeati.it/dettaglio/58610
  2. De viris illustribus, sura 83
  3. Martyrologium Romanum
  4. Patrologia Graeca, XVIII, 27-220.

Marejeo mengine

hariri
  • Froom, LeRoy (1950). The Prophetic Faith of our Fathers. Juz. la 1. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-11-06. Iliwekwa mnamo 2016-06-14. {{cite book}}: Invalid |ref=harv (help)
  • Patterson, L. G. (Lloyd George), Methodius of Olympus: Divine Sovereignty, Human Freedom, and Life in Christ (Washington: Catholic University of America Press, 1997).

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.