Meza (kwa Kilatini na Kiingereza Mensa) [1] ni jina la kundinyota ndogo kwenye angakusi.

Nyota za kundinyota Mesa (Fornax ) katika sehemu yao ya angani
Ramani ya Meza (LMC= Large Magellan Claoud = Wingu Kubwa la Magellan)

Mahali pake

Meza lipo jirani na makundinyota ya Panji (Dorado) upande wa kaskazini, Nyoka Maji (Hydrus) upande wa kaskazini-magharibi na magharibi, Thumni (Octans) upande wa kusini, Kinyonga (Chamaleon) upande wa mashariki halafu Panzimaji (Volans) upande wa kaskazini-mashariki

Jina

Meza ni kati ya makundinyota yaliyoobuniwa katika enzi ya kisasa. Kama ilivyo kwa nyota nyingine zinazoonekana kwenye angakusi pekee haikujulikana kwa Wagiriki wa Kale wala kwa Waarabu. Kwa hiyo wataalamu wa Ulaya hawakuwa na habari nayo. Kundinyota hili lilielezwa mara ya kwanza na Mfaransa Nicolas-Louis de Lacaille wakati wa karne ya 18 kwa jina “Montagne de la Table“ linalomaanisha “Mlima wa Meza“. . Jina la Kifaransa lilitafsiriwa kwa Kilatini na kufupishwa kuwa "Mensa" (Meza). Hapo alitaka kuheshimu mlima aliouangalia kila siku yaani Mlima wa Meza uliopo kwenye mji wa Cape Town.

Lacaille alikaa miaka miwili kwenye Rasi ya Tumaini Jema (Afrika Kusini) alipokuwa akitazama nyota za angakusi ambazo wakati ule zilianza tu kujulikana kati ya wanaastronomia wa Ulaya. Alipima nyota 10,000 akazipanga katika makundinyota na kutunga majina kwa makundinyota mapya 14[2].

Meza lipo katika makundinyota 88 yaliyooorodheshwa na Umoja wa Kimataifa wa Astronomia [3] kwa jina la Mensa. Kifupi chake rasmi kufuatana na Ukia ni 'Men'.[4]

Nyota

Nyota za Meza ni chache na dhaifu sana. Hakuna nyota iliyo na mwangaza juu ya mag 5. Nyota angavu zaidi ni Alpha Mensae yenye mwangaza unaoonekana wa mag 5.09 ikiwa umbali wa miakanuru 33 kutoka Dunia.[5]

Wingu Kubwa la Magellan linapakana na nyota za Meza. Kuwepo kwake kulimhamasisha Lacaille kuchagua jina la "Mlima wa Meza" kwa sababu mlima Cape Town huwa na wingu juu yake.

Tanbihi

  1. Uhusika milikishi (en:genitive) ya neno "Mensa " katika lugha ya Kilatini ni "Mensae" na hili ni umbo la jina linaloonekana katika majina ya nyota za kundi hili kama vile Alfa Mensae, nk.
  2. Histoire de l'Académie royale des sciences ; taarifa ya Lacaille katika "Historia ya Akademia ya Kifalme ya sayansi", uk. 589, Tovuti ya Bibliothèque nationale de France (BnF), iliangaliwa Julai 2017
  3. The Constellations, tovuti ya International Astronomical Union , iliangaliwa Julai 2017
  4. Russell, Henry Norris (1922). "The New International Symbols for the Constellations". Popular Astronomy 30: 469–71. Bibcode:1922PA.....30..469R. 
  5. [ http://simbad.u-strasbg.fr/simbad/sim-basic?Ident=alpha+mensae&submit=SIMBAD+search LTT 2490 -- High proper-motion star"] SIMBAD. Centre de Données astronomiques de Strasbourg. Iliangaliwa Septemba 2017.

Viungo vya Nje

  Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Meza (kundinyota) kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.