Mfalme Amoni

Mfalme Amoni alikuwa mfalme wa Ufalme wa Yuda (643 KK - 641 KK au 642 KK - 640 KK).

Alikuwa mwana wa mfalme Manase na mkewe Meshulemet akafuata uovu wa baba yake.

Alipata kuwa mfalme akiwa na umri wa miaka 22 akatawala kwa miaka 2 tu kwa kuwa aliuawa na watumishi wake (2 Wafalme 21:18-26; 2 Mambo ya Nyakati 33:22).

Mfalme Amoni alimuoa Jedidah, nao walikuwa na mwana aliyeitwa Yosia.

Manase, Amoni na Yosia wametajwa katika vizazi vya ukoo wa Yesu katika Injili ya Mathayo, 1:1-17.

Saint-stub-icon.jpg Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mfalme Amoni kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.