Kitabu cha Pili cha Wafalme
Kitabu cha pili cha Wafalme ni sehemu ya Tanakh (Biblia ya Kiebrania na ya Agano la Kale katika Biblia ya Kikristo. Hugawiwa katika sura 25.
Historia ya kitabuEdit
Zamani kilikuwa kitabu kimoja na Wafalme I lakini katika tafsiri ya Septuaginta kiligawiwa. Wataalamu huamini hii ilitokana na urefu wa kitabu, si kwa sababu za yaliyomo au mpangilio.
Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.
YaliyomoEdit
Kinasimulia habari za sehemu mbili za Israel ya Kale baada ya ugawaji wa milki yaani
- Ufalme wa Israeli katika kaskazini kuanzia mfalme Ahazia hadi mwisho wake wakati wa mfalme Hoshea na kuchukuliwa utumwani kwa makabila ya kaskazini na Waashuri.
- Ufalme wa Yuda katika kusini kuanzia mfalme Ahazia hadi maangamizi ya Yerusalemu na uhamisho wa Babeli.
Viungo vya njeEdit
Mwanzo Kutoka Walawi Hesabu Kumbukumbu Yoshua Waamuzi Ruthu Samueli I Samueli II Wafalme I Wafalme II Mambo ya Nyakati I Mambo ya Nyakati II Ezra Nehemia TobitiDKYudithiDKEsta Wamakabayo IDKWamakabayo IIDKYobu Zaburi Methali Mhubiri Hekima DKSiraDKWimbo Bora Isaya Yeremia Maombolezo BarukuDKEzekieli Danieli Hosea Yoeli Amosi Obadia Yona Mika Nahumu Habakuki Sefania Hagai Zekaria Malaki - Alama ya DK inaonyesha vitabu vya deuterokanoni visivyopatikana katika matoleo yote ya Biblia.
Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kitabu cha Pili cha Wafalme kama historia yake au athari wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |