Maharagwe

(Elekezwa kutoka Maharagwe-mboga)
Maharagwe
(Phaseolus vulgaris)
Makaka mabichi
Makaka mabichi
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Planta (mimea)
(bila tabaka): Angiospermae (Mimea inayotoa maua)
(bila tabaka): Eudicots (Mimea ambayo mche wao una majani mawili)
(bila tabaka): Rosids (Mimea kama mwaridi)
Oda: Fabales (Mimea kama mharagwe)
Familia: Fabaceae (Mimea iliyo na mnasaba na mharagwe)
Jenasi: Phaseolus
Spishi: P. vulgaris
L.

Maharagwe (pia: maharage) ni mbegu za mimea mbalimbali (miharagwe) kutoka familia ya Fabaceae lakini mara nyingi sana Phaseolus vulgaris.

Phaseolus vulgaris”

Mbegu hizi ni zao muhimu la chakula zinazolimwa kote duniani. Kuna spishi mbalimbali zinazojumlisha kati ya mazao ya jamii kunde. Mara nyingi mbegu zinavunwa baada ya kukauka na faida yake ni ya kwamba zinakaa muda mrefu, haziozi haraka.

Kuna aina zinazoweza kuliwa zikiwa bichi kabla ya kukomaa na kupikwa hivyo katika makaka yao: maharagwe-mboga. Kenya inalima aina hii kwa soko la Ulaya zikisafirishwa kwa ndege.

Maharagwe huwa na kiasi kikubwa cha protini. Kwa watu wasiokula nyama, au wana uwezo mdogo tu kujipatia nyama, maharagwe zinatosheleza mahitaji ya protini.

Asili na uenezi

hariri

Mharagwe ni mmea ukuao kwa mwaka mmoja wenye asili ya Amerika ya Kati ya kale na huko Andes, na sasa unalimwa maeneo mengi duniani kwa mbegu zake za maharagwe zinazoliwa, zilizo maarufu zote zikiwa zimeiva na hata zikiwa bado mbichi. Tani milioni 18.3 za maharagwe makavu na nyingine milioni 6.6 za maharagwe mabichi zililimwa mnamo mwaka 2007 duniani kote. Maharagwe ni miongoni mwa vyakula vikuu vya huko Amerika.

Majani yake kwa kawaida hutumika kama mboga na mashina yake hutumika kama chakula cha wanyama.

Kitaalamu, mharagwe upo kwenye kundi la dikotiledoni. Mharagwe hupata naitrojeni kupitia vitundu vilivyopo kwenye mizizi yake, kutokana na kazi ya bakteria ziitwazo rhizobia.

Maharagwe ya kawaida ni spishi kubwa yenye historia ndefu. Mmea wake huwa na ukubwa wa sentimita 20 – 60. Aina zote hutoa majani ya kijani au zambarau, yaliyogawanyika katika sehemu tatu, kila moja likiwa na urefu wa sentimita 6 – 15 na upana wa sentimita 3 – 11. Hutoa maua meupe, ya pinki au ya hudhurungi yenye urefu wa sentimita 1, ambayo hukuwa na kuwa ganda lenye urefu wa sentimita 8 – 20. Ganda hili huweza kuwa na rangi ya kijani, njano, nyeusi au ya hudhurungi, na kila moja huwa na mbegu 4 – 6. Maharagwe huwa laini, yaliyotuna na umbo la mafigo, yakiwa na urefu mapaka wa sentimita 1.5, huku yakiwa na rangi mbalimbali, na mara nyingi huwa na mchanganyiko wa rangi mbili au zaidi.

Aina nyingine ya maharagwe ni haragwe pana, mbegu ya Vicia faba, ambayo tani milioni 3.7 tu zililimwa mwaka 2007. Biashara ya maharagwe imejigawanya vizuri katika nchi za Asia, Afrika, Ulaya, Oceania, Amerika ya Kusini na Amerika ya Kaskazini. Brazili ndiyo wazalishaji wakuu wa maharagwe makavu huku China wakiwa ndiyo wazalishaji wakuu wa maharagwe mabichi, kwa wastani sawa na wazalishaji kumi wote waliobakia kwa pamoja.

Maharagwe makavu

hariri

Sawa na maharagwe mengine, haya huwa na kiasi kikubwa cha wanga, protini, na makapi na ni chanzo kizuri cha madini ya chuma, potasiamu, seleniamu, molibediamu, thayamaini, vitamini B6 na asidi ya foliki.

Maharagwe haya yatadumu na virutubisho vyake kama yatatunzwa kwenye sehemu kavu na isiyo na joto kali. Lakini kwa kadiri yanavyokaa kwa muda mrefu, virutubisho na ladha yake hupungua na hata muda wa kupika huongezeka.

Mapishi

hariri

Maharagwe haya mara zote hupikwa kwa kuchemshwa, na mara zote kwa masaa kadhaa. Wakati kulowekwa kwenye maji si lazima muda wote, hupunguza muda wa kupika, kuboresha pishi na kupekea mmeng’enyo rahisi wa chakula.

Kuna namna mbalimbali za upishi wa maharagwe, pamoja na ile ya kuloweka maharagwe usiku kucha, au ile ya kuchemsha maharagwe kwa dakika tatu tu na kisha kuyaloweka kwa masaa 2 – 4, na kisha kuyakausha na kuendelea na upishi. Maharagwe ya kawaida huchukua muda mrefu kupika, kuanzia saa 1 – 4 hivi, lakini hutofautiana kutoka aina moja mpaka nyingine.

Huko Meksiko, Amerika ya Kati na Amerika ya Kusini, chakula cha asili cha maharagwe ni epazote, ambacho husemekana kuongeza mmeng’enyo wa chakula.

Maharagwe pia yanaweza kununuliwa yakiwa yamekwishapikwa tayari, na kuuzwa kwenye makopo.

Hata hivyo kuna aina kadhaa za maharagwe kama zinavyoonyeshwa hapo chini.

  Makala hii kuhusu mmea fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Maharagwe kama uainishaji wake wa kibiolojia, uenezi au matumizi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.