Milima ya Nuba (kwa Kiarabu جبال النوبة jabal an-nuba) ni eneo lililo katika Kordofan Kusini, Sudan. Eneo hilo ni nyumbani kwa kundi la makabila ya asili yanayojulikana kwa pamoja kama Wanuba.

Milima ya Nuba
Ramani ya Sudan (baada ya 2011). "Nuba Mountains" inaandikwa katika Kordofan Kusini.

Historia

hariri

Katika karne ya 18 eneno lilikuwa chini ya wafalme wa Wanuba waliojulikana kama Taqali, walioshindwa na Dola la Mahdi. Wakati ule wahamiaji Waarabu wengi Wabaggara waliingia katika maeneo ya Kordofan Kusini.

Hadi sasa watu milioni 1.5 wanaishi katika milima hiyo, hasa kabila la Nuba na wachache wa Wabaggara. [1]

Jiografia

hariri

Milima inaenea kilomita 64 kwa 145 ikifikia kimo cha mita 450 hadi 900 juu ya UB.[2] Tabianchi ni ya kitropiki, joto na nusu-yabisi inayopokea kwa wastani milimita 300 hadi 800 za mvua kwa mwaka. Wakati wa kiangazi kinachoendelea kuanzia Februari hadi Mei mara nyingi kuna uhaba wa maji. [3]

Marejeo

hariri
  1. "Nuba Mountains". Bradt Guides. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-12-11. Iliwekwa mnamo 2021-12-11.
  2. "BBC News - Will Sudan's Nuba Mountains be left high and dry?". bbc.co.uk.
  3. Ahmed, F.; Hagaz, Y.A.; Andrawis, A.S. (1984). "Landsat model for groundwater exploration in Nuba Mountains, Sudan". Advances in Space Research. 4 (11): 123–131. Bibcode:1984AdSpR...4k.123A. doi:10.1016/0273-1177(84)90400-9.

Viungo vya nje

hariri