Milki ya Maurya
Milki ya Wamaurya (kwa Kiing. Maurya Empire) ilikuwa milki kubwa ya kwanza katika historia ya Uhindi. Mlki hiyo ilianzishwa mnamo 322 KK na Chandragupta Maurya.
Utawala wa Chandragupta Maurya
haririChandragupta Maurya alianzisha milki ya Maurya kwa kupindua nasaba ya Nanda na kupanua ufalme huo kwa msaada wa Chanakya. Kufikia 316 KK, himaya ya Maurya ilitawala kabisa sehemu za Kaskazini-Magharibi za Uhindi, ikiwashinda na kuteka maeneo yaliyokuwa chini ya magavana walioachwa na Aleksander Mkuu. Chandragupta Maurya alimshinda Seleukus I Nikator akapata maeneo upande wa magharibi wa Mto Indus. [1]
Baada ya Chandragupta Maurya, mwanawe Bindusara alianza kutawala kutoka 298 KK. Aliitwa "Amitraghata", neno la Kisanskrit linalomaanisha kwamba Bindusara ndiye "muuaji wa maadui". Alishinda sehemu za kusini mwa Uhindi. Baada ya kifo chake, ni Kalinga tu (Orissa wa kisasa) na sehemu za Tamil Nadu zilizobaki nje ya himaya yake.
Kipindi cha dhahabu cha milki
haririMfalme Ashoka, mwana wa Bindusara, alikuwa mtawala wa Milki ya Maurya mnamo 268 KK. Anahesabiwa kati ya watawala mashuhuri zaidi wa Bara Hindi. Ashoka alishinda Kalinga katika vita kali inayojulikana kama Vita ya Kalinga. Hii ndiyo vita pekee iliyopigwa na Mfalme Ashoka. Waliokufa ni zaidi ya watu 200,000. Mkoa wa Kalinga uliharibiwa na ulionekana umwagaji damu. Hii ilibadilisha mawazo ya Ashoka. Alijitolea maisha yake yote kwa "ahinsa" na "dharma-vijaya". Akawa Mbudha baada ya vita hivi. Amri zake zimehifadhiwa kama mwandishi uliochongwa katika miamba kwenye milki yake.
Nembo ya kisasa ya Uhindi ilinakiliwa kutoka kwa moja ya nguzo zake za mwamba. Kwa kawaida aliitwa Ashoka Mkuu.
Kushuka
haririBaada ya kifo cha Ashoka mnamo 232 KK, milki yake ilianza kupungua. Dola hilo lilidumu miaka hamsini tu baada ya kifo chake. Brihadratha Maurya, mfalme wa mwisho wa Wamaurya aliuawa na jenerali wake Pushyamitra Sunga, ambaye alianzisha Milki ya Sunga mnamo 185 KK. [2]
Marejeo
hariri- ↑ http://www.metmuseum.org/toah/hd/maur/hd_maur.htm
- ↑ "KING ASHOKA: His Edicts and His Times". www.cs.colostate.edu.