Mjenzi (kutoka kitenzi "kujenga", ambacho kwa asili kinahusu nyumba za miti, lakini sasa aina zote za majengo) ni mtu ambaye amebobea katika mambo ya ujengaji wa majengo ya aina mbalimbali kama nyumba, hata za maghorofa, shule, hospitali, maabadi, madaraja na mengineyo.

Wajenzi.
Mjenzi
Hatari kazini.
Matokeo ya kazi ya wajenzi.

Mjenzi hutumia zana mbalimbali kujengea (kwa pamoja huitwa vifaa vya ujenzi). Zana hizo ni kama vile tindo, nyundo, sepeto na vifaa vya kujengea kama miti, udongo, sementi, chokaa, mchanga, mitambo ya ujenzi na vinginevyo. Mara nyingi wajenzi huvaa vifaa vya kujilinda kama vile kofia ngumu na mabuti ya kazi yenye chuma ili kulinda vidole na katika nchi fulani vifaa hivyo vinatakwa na sheria.

Siku hizi mjenzi kwa kawaida anafuata ramani ambayo imechorwa na mhandisi halafu imepitishwa na mamlaka ya serikali, ili kujenga vitu kwa vipimo na mahesabu.

Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mjenzi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.