Mjusi-kafiri mchana

(Elekezwa kutoka Mjusi wa mnazi)
Mjusi-kafiri mchana
Mjusi-kafiri mchana pwani (Phelsuma dubia)
Mjusi-kafiri mchana pwani (Phelsuma dubia)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Reptilia (Wanyama wenye damu baridi na magamba ngozini)
Oda: Squamata (Mijusi, mijusi-nyungunyungu na nyoka)
Nusuoda: Lacertilia (Mijusi)
Oda ya chini: Gekkota (Mijusi-kafiri)
Familia: Gekkonidae (Mijusi-kafiri wa kawaida)
Gray, 1825
Jenasi: Phelsuma (Mijusi-kafiri mchana)
Gray, 1825
Ngazi za chini

Spishi 53:

Mijusi-kafiri mchana ni mijusi wa jenasi Phelsuma katika familia Gekkonidae. Kinyume na spishi nyingine za mijusi-kafiri, ambazo hukiakia usiku, spishi hizi hukiakia mchana. Katika Unguja na Pemba spishi za huko huitwa mijusi wa mnazi pia, kwa sababu wanatokea kwa majani ya minazi.

Takriban mijusi wote wa jenasi hii wana rangi ya majani. Wengine ni buluu, kijivu au kahawia. Mara nyingi wana madoa na/au milia mekundu, buluu, njano au meusi.

Spishi nyingi ni ndogo kuliko mijusi-kafiri wengine, k.m. chini ya sm 15. Ile ndogo kabisa ni mjusi-kafiri mchana kibete, ambaye inafika sm 7.1 tu. Spishi nyingine zinafika sm 30 na mjusi-kafiri mkubwa wa Rodrigues, ambaye amekwisha sasa, alikuwa na urefu wa hadi sm 40.

Mijusi hawa hula wadudu, vertebrata wengine, mbochi, mbelewele na matunda mororo.

Spishi

hariri

Marejeo

hariri
  • Spawls, S., Howell, K., Drewes, R. & Ashe, J. (2002) A field guide to the Reptiles of East Africa. Academic Press, San Diego, CA, USA.

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mjusi-kafiri mchana kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.