Mlandanisho
Katika utarakilishi, mlandanisho (kwa Kiingereza: Synchronization) unahusu vitu viwili: mlandanisho wa michakato na mlandanisho wa data.
- Mlandanisho wa michakato ni michakato mingi inapoungana ili kufanya kitendo kimoja.
- Mlandanisho wa data ni kuzinakili na kuzibandika data katika vifaa vya kutunzia vingi kama wingu (mtandao) au diski kuu.

Mchoro wa mlandanisho.
MarejeoEdit
- Kahigi, K. K. (2007). Ujanibishaji wa Office 2003 na Windows XP kwa Kiswahili Sanifu. Kioo cha Lugha, 5(1).