Mlangobahari wa Bass
Mlangobahari wa Bass (kwa Kiingereza Bass Strait) ni sehemu nyembamba ya Bahari Pasifiki inayotenganisha Tasmania na bara la Australia (eneo la jimbo la Victoria).
Mlangobahari huo una upana wa kilomita 240 na maji huwa na kina cha mita 50 kwa wastani. Kuna visiwa vingi ndani yake pamoja na visiwa vya King Island na Flinders Island.
Jina la mlangobahari limetokana na Mwingereza George Bass aliyepita hapa mwaka 1798.[1]
Kuna dhoruba nyingi na mawimbi makubwa, hivyo jahazi na meli nyingi zilipotea wakati wa karne ya 19. Kwa hiyo minara ya taa ilijengwa kwenye visiwa mbalimbali na rasi za pwani kuanzia mwaka 1848.
Marejeo
hariri- ↑ Flinders, Matthew (1814). A Voyage to Terra Australis
Viungo vya Nje
haririWikimedia Commons ina media kuhusu: