Mlangobahari wa Davis

Mlangobahari wa Davis (kwa Kiingereza: Davis Strait) ni mkono wa kaskazini wa Bahari ya Labrador. Mlangobahari huu unaunganisha Bahari ya Labrador upande wa kusini na Hori ya Baffin upande wa kaskazini. Unatenganisha Greenland upande wa mashariki na Kisiwa cha Baffin cha Nunavut, Kanada, upande wa magharibi.

Mlangobahari wa Davis iko baina ya Greenland and Kisiwa cha Baffin, Kanada.     Nunavut     Quebec     Newfoundland na Labrador     Maeneo nje ya Kanada (Greenland, Iceland)
Pwani ya mlangobahari wa Davis katika Greenland.

Jina linatokana na Mwingereza John Davis (15501605), aliyepeleleza eneo hili alipotafuta njia ya kaskazini-magharibi kati ya bahari za Atlantiki na Pasifiki katika karne ya 16.

Kina cha maji hufikia mita 2,000.

Viungo vya NjeEdit

Wikimedia Commons ina media kuhusu:

Majiranukta kwenye ramani: 65°N 58°W / 65°N 58°W / 65; -58 (Davis Strait)


  Makala hii kuhusu maeneo ya Kanada bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mlangobahari wa Davis kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.