Mlangobahari wa Denmark

Mlangobahari wa Denmark (kwa Kiingereza: Denmark Strait au Greenland Strait; kwa Kidenmark: Danmarksstrædet; kwa Kiiceland: Grænlandssund) ni sehemu ya Bahari Atlantiki inayotenganisha Greenland upande wa kaskazini na Iceland upande wa kusini. Kisiwa cha Jan Mayen cha Norwei kiko upande wa mashariki wa mlangobahari huo.

Ramani ya Bahari ya Norwei.
Mapande ya barafu katika Mlangobahari wa Denmark.

Mlangobahari wa Denmark unaunganisha Bahari ya Greenland (sehemu ya Bahari Aktiki) na Bahari Atlantiki. Una urefu wa kilomita 480 na upana wa km 290.

Upande wa magharibi wa mlangobahari huo kuna maporomoko makubwa chini ya uso wa bahari ambako maji baridi kutoka Aktiki hushuka zaidi ya mita 3,000 kuelekea vilindi vya Atlantiki. Maporomoko hayo ni sehemu muhimu ya mzunguko wa maji wa Atlantiki.

Wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia, tarehe 24 Mei 1941, yalitokea mapigano ya baharini baina ya manowari kubwa "Bismarck" ya Ujerumani na manowari za Uingereza.


Coordinates: 67°N 24°W / 67°N 24°W / 67; -24