Mlipuko wa homa ya mafua wa 1918
Mlipuko wa homa ya mafua wa 1918 (unaojulikana pia kama Spanish Flu) ulikuwa pandemia ya homa ya mafua iliyotokea kwenye mwisho wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia. Ulidumu miaka mitatu, kuanzia Januari 1918 hadi Desemba 1920. [1] Takriban watu milioni 500[2] waliambukizwa duniani kote ilhali wakati ule idadi ya watu duniani ilikuwa milioni 1,800 tu.
Ugonjwa uliosambaa shauri ya Vita Kuu
haririUsambazaji wake uliathiriwa na vita ambako wanajeshi na wafanyakazi walisafirishwa kwa idadi kubwa kati ya mabara yote, pia kutokana na njaa iliyosambaa katika sehemu nyingi za dunia wakati wa vita na kudhoofisha watu wengi.
Pandemia hiyo iliua baina ya watu milioni 50 hadi 100[3] - waliokuwa sawa na asilimia 3 hadi 5 ya watu wote duniani wakati huo. [3] Hii inamaanisha kuwa lilikuwa moja ya maafa asilia mabaya zaidi katika historia. [2] [4] [5] [6]
Jina la "Spanish Flu"
haririJina "mafua ya Kihispania" (Spanish Flu) lilitokana na taarifa juu ya ugonjwa katika magazeti ya Hispania; hali halisi nchi nyingine za Ulaya ziliathiriwa vibaya zaidi lakini serikali za nchi zilizoshiriki vitani zililenga kuficha habari za vifo vingi [7] [8]; ilhali Hispania haikushiriki vita, hivyo magazeti yalikuwa na uhuru. Kwa hiyo taarifa katika magazeti yake yalileta picha isiyo ya kweli kuwa ugonjwa ulianza Hispania[9].
Tabia za ugonjwa
haririVirusi vilisambaa duniani kwa mawimbi matatu. Wimbi la kwanza mwanzoni wa mwaka 1918 halikuwa na nguvu sana, na pale lilipopita watu walianza kujenga kinga dhidi ya mawimbi yaliyofuata. Wimbi kuu lilianza kwenye Oktoba/Novemba 1918 na kuua watu wengi. Iliathiri zaidi Afrika ambako wimbi la kwanza halikufika. Wimbi la tatu liliendelea hadi 1920 lakini halikuwa kali vile kwa sababu watu wengi waliwahi kuambukizwa na hivyo kuwa na kinga[10].
Tabia ya pekee ya pandemia hiyo ilikuwa kwamba homa ya mafua kwa kawaida inasababisha vifo kati ya watoto wadogo na wazee, lakini mlipuko huo uliua hasa vijana na watu wazima wenye umri wa wastani.
Hakuna data za kutosha ili kuhakikisha mahali ambapo ugonjwa huo ulipoanzia. [2] Virusi vyake vilikuwa vya aina H1N1. Mabadiliko ya aina hiyo yalirudi katika karne ya 20 na 21 yakisabisha pandemiki mpya.
Athari katika Afrika ya Mashariki
haririTanganyika iliona mapigano kwa miaka yote ya Vita Kuu hadi Novemba 1918. Wanajeshi kutoka nchi jirani kama Kenya, Rhodesia (Zambia) na Kongo, kutoka Afrika Kusini, Ulaya na Uhindi waliingia na kurudi na kusambaa virusi vyake, pamoja na wapagazi elfu nyingi waliolazimishwa kubeba mizigo yao. Mapigano yaliwahi kuleta uharibifu na njaa ilhali askari walichukua vyakula vyote walivyokuta katika nchi ambako ukosefu wa barabara ulileta ugumu wa kupeleka vyakula hadi vikosi kwenye pori.
Maambukizi ya kwanza yalitambuliwa Mombasa, Kenya mnamo Septemba 1918[11]. Ugonjwa ulifika kwa meli kutoka Uhindi. Kutoka hapa ulisambaa haraka pamoja na wapagazi wa Carrier Corps walioachishwa na kubeba virusi hadi makwao nyumbani.[12]
Virusi vilienea haraka hadi Tanganyika iliyotawaliwa wakati ule na majeshi wa Uingereza na Ubelgiji, ilhali vikosi vya Wajerumani walipatikana kwenye kanda nyembamba la kusini. Waingereza walipoanza kujenga serikali yao kwenye mwisho wa 1918, walikadiria kuwa nusu ya watu wote aliathiriwa. Katika eneo la Tukuyu lenye wakazi 180,000, takriban asilimia 10 au watu 18,000 walikufa. Makadirio ya vifo vyote katika Tanganyika hutaja vifo 100,000 (eneo lote lilikuwa na wakazi milioni 4 kabla ya vita). Zanzibar pekee iliweza kuthibiti mlipuko kwa sababu serikali ilichukua hara hatua za kutenganisha wagonjwa na kuwafuatilia.[13]
Picha
hariri-
Wauguzi wawili wa Msalaba Mwekundu wa Marekani walionyesha mazoea ya matibabu wakati wa janga la homa ya 1918.
-
Wakulima wa Alberta (Kanada) walivaa barakoa kujikinga na homa ya mafua.
-
Polisi wakiwa wamevaa barakoa zilizotolewa na Shirika la Msalaba Mwekundu la Marekani huko Seattle, 1918
-
Wafanyakazi wa Msalaba Mwekundu wakimwondoa mwathirika wa homa huko St. Louis, Missouri (1918)
-
Wodi ya homa ya mafua katika Hospitali ya Walter Reed wakati wa 1918-1919
-
Kuzika wahanga wa homa ya mafua, North River, Kanada (1918)
-
1919 Tokyo, Japan
Marejeo
hariri- ↑ Taubenberger JK; Morens DM 2006. "1918 Influenza: The Mother of All Pandemics" (PDF). Emerging Infectious Diseases. 12 (1): 15–22. doi:10.3201/eid1201.050979. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo Mei 2, 2020. Iliwekwa mnamo Februari 4, 2016.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: multiple names: authors list (link) CS1 maint: numeric names: authors list (link) - ↑ 2.0 2.1 2.2 Taubenberger JK; Morens DM 2006. "1918 Influenza: The Mother of All Pandemics" (PDF). Emerging Infectious Diseases. 12 (1): 15–22. doi:10.3201/eid1201.050979. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo Mei 2, 2020. Iliwekwa mnamo Februari 4, 2016.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: multiple names: authors list (link) CS1 maint: numeric names: authors list (link) - ↑ 3.0 3.1 "Historical Estimates of World Population". United States Census Bureau. United States Department of Commerce. Julai 9, 2015. Iliwekwa mnamo Februari 4, 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Patterson KD; Pyle GF 1991. "The geography and mortality of the 1918 influenza pandemic". Bulletin of the History of Medicine. 65 (1). Johns Hopkins University: 4–21. PMID 2021692.
{{cite journal}}
: CS1 maint: multiple names: authors list (link) CS1 maint: numeric names: authors list (link) - ↑ Billings, Molly (Juni 1997). "The Influenza Pandemic of 1918". virus.stanford.edu. Stanford University. Iliwekwa mnamo Februari 4, 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Johnson NP; Mueller J 2002. "Updating the accounts: Global mortality of the 1918–1920 "Spanish" influenza pandemic". Bulletin of the History of Medicine. 76 (1): 105–15. doi:10.1353/bhm.2002.0022. PMID 11875246.
{{cite journal}}
: CS1 maint: multiple names: authors list (link) CS1 maint: numeric names: authors list (link) - ↑ Valentine, Vikki (Agosti 20, 2008). "Origins of the 1918 Pandemic: The Case for France". NPR.org. National Public Radio (NPR). Iliwekwa mnamo Februari 4, 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Anderson, Susan (Agosti 29, 2006). "Analysis of Spanish flu cases in 1918–1920 suggests transfusions might help in bird flu pandemic". EurekAlert.org: The Global Source for Science News. American College of Physicians. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-11-25. Iliwekwa mnamo Feb 4, 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Barry, John M. (2004). The Great Influenza: The Epic Story of the Greatest Plague in History. Viking Penguin. uk. 171. ISBN 0-670-89473-7.
- ↑ Lessons from the 1918-1919 Spanish Flu Pandemic in Africa, tovuti ya Africa Center for Strategic Studies, May 13, 2020, iliangaliwa Novemba 2021
- ↑ https://www.mdpi.com/2414-6366/4/2/91/htm Impact of the 1918 Influenza Pandemic in Coastal Kenya, rop. Med. Infect. Dis. 2019, 4(2), 91; https://doi.org/10.3390/tropicalmed4020091
- ↑ https://encyclopedia.1914-1918-online.net/article/influenza_pandemic_africa Influenza Pandemic (Africa), tovuti ya 1914-1918 online
- ↑ https://www.linkedin.com/pulse/how-covid-19-giving-east-africa-sense-d%C3%A9j%C3%A0-vu-fredrick-boshe How COVID-19 is giving East Africa a sense of Déjà Vu, blogu ya F Boshe, iliangaliwa Novemba 2021