Modesti wa Yerusalemu

Modesti wa Yerusalemu (Sivas, Kapadokia, leo nchini Uturuki, karne ya 617 Desemba 630[1]) alikuwa askofu wa mji huo nchini Israeli.

Masalia ya Mt. Modesti wa Yerusalemu panapotunzwa.

Kabla ya hapo aliuzwa kama mtumwa kwenda Misri. Huko alimuongoa bwana wake ambaye alimuacha huru. Hapo alijiunga na umonaki kwenye mlima Sinai. Baada ya kufanywa abati wa monasteri huko Palestina.

Mwaka 614 Kosroe II wa Persia aliteketeza Yerusalemu akiua Wakristo 66,509. Modesti alichaguliwa kushika nafasi ya askofu Zakaria aliyetekwa, na huyo alipofariki Modesti akawa askofu. Alijitahidi kujenga upya monasteri na makanisa[2].

Tangu kale ametambuliwa kuwa mtakatifu.

Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe 17 Desemba[3].

Tazama piaEdit

TanbihiEdit

Viungo vya njeEdit

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.