Moma
Moma wa kawaida au bafe Bitis arietans
Moma wa kawaida au bafe
Bitis arietans
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Reptilia (Wanyama wenye damu baridi na magamba ngozini)
Oda: Squamata (Mijusi, mijusi-nyungunyungu na nyoka)
Nusuoda: Serpentes (Nyoka)
Oda ya chini: Alethinophidia (Nyoka wasio vipofu)
Familia: Viperidae (Nyoka walio na mnasaba na kipiri)
Oppel, 1811
Jenasi: Bitis
Gray, 1842
Ngazi za chini

Spishi 18:

Moma ni spishi za nyoka wenye sumu wa jenasi Bitis katika familia Viperidae. Spishi moja huitwa bafe pia na spishi nyingine wa familia Viperidae huitwa vipiri.

Spishi nyingi za moma, zile za Afrika ya Mashariki hasa, ni kubwa na nene kuliko vipiri wengine, lakini spishi kadhaa ni ndogo zaidi na moma mdogo wa Namakwa ni mdogo kabisa wa Viperidae wote duniani. Kinyume chake moma-misitu ni mkubwa kabisa.

Wakitishwa moma hutuna na kujipojaa wakifyonya kwa sauti kubwa. Inaonekana kama sio wepesi lakini wanaweza kupiga kwa kasi ya umeme.

Nyoka hawa ni wanene na wazito kwa kulinganisha na urefu wao. Wana kichwa kipana kwa umbo wa pembetatu na mkia mfupi. Magamba yao yana miinuko na yale ya pua yanaweza kuwa marefu na kufanana na pembe.

Spishi

hariri

Marejeo

hariri
  • Spawls, S., Howell, K., Drewes, R. & Ashe, J. (2002) A field guide to the Reptiles of East Africa. Academic Press, San Diego, CA, USA.

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Moma kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.