Monegunda
Monegunda (alifariki Tours, Ufaransa, 3 Juni 570) alikuwa mwanamke Mkristo ambaye baada ya kuolewa na kuzaa watoto wa kike waliowahi kufariki akawa mkaapweke kwa ruhusa ya mume wake[1].
Kwanza aliishi kwao Chartres, halafu akahamia sehemu za Tours ambako alipata wafuasi hadi ikaanzishwa monasteri[2].
Habari zake zimeandikwa na Gregori wa Tours ambaye alimfahamu.
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Tazama pia
haririMarejeo
hariri- ↑ "St. Monegundis - Saints & Angels - Catholic Online". Catholic Online. Iliwekwa mnamo 2016-07-28.
- ↑ https://www.santiebeati.it/dettaglio/60420
- ↑ Martyrologium Romanum
Viungo vya nje
haririMakala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |