Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi(Moshi Co-operative University (MoCU)) ni chuo kikuu kilichoko Moshi, Tanzania. Ni chuo kikuu kinachojikita katika kutoa elimu inayohusiana na ushirika na masuala ya uchumi wa ushirika. Chuo hichi kina lengo la kuwapa wanafunzi maarifa na stadi zinazohitajika kushiriki kikamilifu katika sekta ya ushirika na maendeleo ya uchumi wa nchi.

Historia

hariri

Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi kilianzishwa rasmi tarehe 5 Januari 1963. Lengo la kuanzishwa chuo lilikuwa kutoa mafunzo kwa rasilimali watu katika sekta ya ushirika ambacho kilikuwa kitengo katika wizara ya Ushirika na Maendeleo ya jamii[1].

Chuo kilianzishwa na sheria ya ushirika namba 32 (kwa sasa imeshabadilishwa) ya mwaka 1964, kikiwa kama taasisi inayojitegemea na utawala wake.

Mwaka 2004, kilifanywa kuwa chuo kikuu kishiriki chini ya Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine.

Mwaka 2014, chuo kikapewa mamlaka kamili ya kuwa chuo kikuu na waziri mstaafu Al Noor Kassum akiwa mkuu wa chuo[2].

Taaluma

hariri

Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi kinatoa shahada, stashahada na astashahada katika fani zifuatazo:

Shahada

hariri
  • Shahada ya Sanaa ya Uhasibu na Fedha
  • Shahada ya Sheria

Stashahada

hariri

Astashahada

hariri

Marejeo

hariri
  1. "Orodha ya Vyuo Vikuu" (PDF). Tanzania Commission for Universities. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 24 Septemba 2015. Iliwekwa mnamo 15 Julai 2013.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi" (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-11-02. Iliwekwa mnamo 2019-11-02.
  Makala hii kuhusu mambo ya elimu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.