Majimbo ya Afrika Kusini

Majimbo ya Afrika Kusini ni ngazi ya kwanza ya ugatuzi nchini Afrika Kusini. Nchi imegawanywa katika majimbo tisa. [1] Katika mkesha wa uchaguzi mkuu wa 1994 nchi ilikuwa na majimbo manne halafu kulikuwa na maeneo ya bantustan. Kabla ya uchaguzi huo wa kwanza ulioendeshwa bila ubaguzi wa rangi maeneo ya bantustan yaliunganishwa tena kisheria na Afrika Kusini na nchi yote iligawiwa kwa majimbo tisa.

Majimbo ya Afrika Kusini

Historia

 
Majimbo manne wakati wa kuunda Muungano wa Afrika Kusini mnamo mwaka 1910

Muungano wa Afrika Kusini ulianzishwa mwaka 1910 kwa kukuunganisha makoloni manne ya Uingereza: Koloni la Rasi, Koloni ya Natal, Koloni ya Transvaal na Koloni ya Mto Orange (hizi mbili za mwisho zilikuwa hadi uvamizi wa Uingereza jamhuri huru za Makaburu zilizojulikana). Makoloni haya yakawa majimbo manne asilia ya Muungano: Mkoa wa Cape, Mkoa wa Transvaal, Mkoa wa Natal na Dola Huru la Oranje .

 
Majimbo na maeneo ya bantustan kama ilivyokuwa mwisho wa ubaguzi wa rangi

Wakazi wasio Wazungu walibanwa katika maeneo maalum kuanzia mwaka 1913. Umiliki wa ardhi kwa watu weusi ulizuiliwa kwa maeneo fulani ya jumla ya 13% ya nchi yote. Kuanzia mwishoni mwa miaka ya 1950, maeneo haya yalibadilishwa hatua kwa hatua kuwa "homelands" au "bantustan". Nne kati ya nchi hizi zilitangazwa kama nchi za pekee za watu weusi wakati wa enzi ya apartheid . Mnamo 1976, nchi ya Transkei ilikuwa ya kwanza kukubali uhuru kutoka kwa Afrika Kusini, na ingawa uhuru huu haukuwahi kutambuliwa na nchi nyingine yoyote, nchi zingine tatu. – Bophuthatswana (1977), Venda (1979) na Ciskei (1981) – zilifuata kukubali uhuru bandia.

Tarehe 27 Aprili 1994, tarehe ya uchaguzi wa kwanza usio wa ubaguzi wa rangi ambako pia Katiba ya Muda ilipitishwa, majimbo haya yote na nchi za bantustan zilivunjwa, na majimbo tisa mapya yalianzishwa. [2]

Orodha

Jimbo Jina kwa lugha inayotumiwa zaidi jimboni Mji mkuu Mji mkubwa Eneo[3]:9 Wakazi

(2022)[4]
Densiti

(2022)
Ramani
Eastern Cape iMpuma-Koloni (Kixhosa) Bhisho (Bisho) Gqeberha (Port Elizabeth) 168,966 km2
(65,238 sq mi)
6,676,691 39.5/km2
(102/sq mi)
 
Free State Freistata (Kisotho) Bloemfontein Bloemfontein 129,825 km2
(50,126 sq mi)
2,921,611 22.5/km2
(58/sq mi)
 
Gauteng eGoli (Kizulu) Johannesburg Johannesburg 18,178 km2
(7,019 sq mi)
16,098,571 885.7/km2
(2,294/sq mi)
 
KwaZulu-Natal iKwaZulu-Natali (Kizulu) Pietermaritzburg Durban 94,361 km2
(36,433 sq mi)
11,538,325 122.3/km2
(317/sq mi)
 
Limpopo Limpopo (Kisotho) Polokwane (Pietersburg) Polokwane 125,754 km2
(48,554 sq mi)
5,941,439 47.2/km2
(122/sq mi)
 
Mpumalanga iMpumalanga (Kiswazi) Mbombela (Nelspruit) Mbombela 76,495 km2
(29,535 sq mi)
4,720,497 61.7/km2
(160/sq mi)
 
North West Bokone Bophirima (Kitswana) Mahikeng (Mafikeng) Rustenburg 104,882 km2
(40,495 sq mi)
4,186,984 39.9/km2
(103/sq mi)
 
Northern Cape Noord-Kaap (Kiafrikaans) Kimberley Kimberley 372,889 km2
(143,973 sq mi)
1,308,734 3.5/km2
(9.1/sq mi)
 
Western Cape Wes-Kaap (Kiafrikaans) Cape Town Cape Town 129,462 km2
(49,986 sq mi)
7,212,142 55.7/km2
(144/sq mi)
 
Republic of South Africa iRiphabhuliki yaseNingizimu Afrika (Kizulu) Pretoria,

Bloemfontein

Cape Town[5]
Johannesburg 1,220,813 km2
(471,359 sq mi)
60,604,992 49.6/km2
(128/sq mi)
 

Tanbihi