Mrungi
(Catha edulis)
Mrungi huko Yemen
Mrungi huko Yemen
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Planta (mimea)
(bila tabaka): Angiospermae (Mimea inayotoa maua)
(bila tabaka): Eudicots (Mimea ambayo mche wao una majani mawili)
(bila tabaka): Rosids (Mimea kama mwaridi)
Oda: Celastrales (Mimea kama mkurufu)
Familia: Celastraceae (Mimea iliyo na mnasaba na mkurufu)
Jenasi: Catha
Forssk. ex Scop.
Spishi: C. edulis
(Vahl) Forssk. ex Endl.

Mrungi, murungu au mlonge (lakini ni afadhali kutumia jina hilo la mwisho kwa Moringa oleifera) ni kichaka au mti mdogo wa familia Celastraceae.

Mrungi hukua kama kichaka au mti mdogo wa urefu wa mita 1-5 na wakati mwingine huweza kufika urefu wa mita 10 penye tabianchi ya ikweta.

Kwa kawaida mmea huo unakua katika mazingira yenye ukame, kwa kiwango cha joto la 5-35°C (41-95°F).

Majani yake ni ya rangi ya kijani, yenye urefu wa sentimeta 5-10 (inchi 2-4) na upana wa sentimeta 1-4 (inchi 0.39-1.6).

Majani na vitawi vyake huitwa miraa na hutafunwa kama kichocheo cha neva.

Picha hariri

  Makala hii kuhusu mmea fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mrungi kama uainishaji wake wa kibiolojia, uenezi au matumizi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.