Msikiti wa Gaddafi, Dodoma
Msikiti wa Gaddafi ndio msikiti mkubwa zaidi nchini Tanzania na wa pili kwa ukubwa Afrika Mashariki baada ya Msikiti wa Kitaifa wa Uganda nchini Uganda. Uko katika mji mkuu wa Tanzania wa Dodoma. Uko katika majira nukta 6°10′22″S 35°44′45″E / 6.172689°S 35.745721°E
Ulipewa jina la Kiongozi wa zamani wa Libya Muammar Gaddafi ambaye alitoa fedha kwa ajili ya ujenzi wake kupitia Jumuiya ya Ulimwengu ya Miito ya Kiislamu. Msikiti huo ulizinduliwa na Rais Jakaya Kikwete mwaka 2010 na una uwezo wa kuchukua waumini wasiopungua 3,000. [1]
Angalia pia
haririMarejeo
hariri- ↑ MSANGYA, DANIEL (5 Machi 2011). "Gaddafi "gifts" to Tanzania in limbo". africareview.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-09-25. Iliwekwa mnamo 6 Julai 2013.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)