Mstahili heshima
Mstahili heshima (kwa Kilatini Venerabilis, kwa Kiingereza Venerable) ni jina ambalo katika Kanisa Katoliki linatumika hasa kwa muumini aliyefariki ambaye, baada ya kesi kuchunguza uadilifu wake wa kiwango cha ushujaa, Papa ameuthibitisha rasmi.
Uchunguzi huo unahusu maadili ya Kimungu (imani, tumaini na upendo), maadili bawaba (busara, haki, nguvu na kiasi) pamoja na unyenyekevu. Kwa watawa unachunguzwa pia utekelezaji wa nadhiri zao.
Pamoja na hayo, Kanisa linasubiri Mungu athibitishe mwenyewe kwa muujiza mmoja iliyopatikana kwa maombezi ya huyo ili aweze kutangazwa mwenye heri na wa pili ili atangazwe mtakatifu.
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mstahili heshima kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |