Mswaki (mti)

(Elekezwa kutoka Msuake)
Mswaki
(Salvadora persica)
Mswaki katika Pakistani
Mswaki katika Pakistani
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Plantae (Mimea)
(bila tabaka): Angiospermae (Mimea inayotoa maua)
(bila tabaka): Eudicots (Mimea ambayo mche wao una majani mawili)
(bila tabaka): Rosids (Mimea kama mwaridi)
Oda: Brassicales (Mimea kama kabichi)
Familia: Salvadoraceae (Mimea iliyo na mnasaba na mswaki)
Jenasi: Salvadora
Spishi: P. persica
L.

Mswaki au msuake ni majina ya miti mbalimbali wa familia Salvadoraceae, lakini spishi kuu iitwayo majina haya ni Salvadora persica. Spishi nyingine ni Dobera glabra na D. loranthifolia zinazoitwa msega na mkupa pia. Miti hii inatokea maeneo makavu ya Afrika na Mashariki ya Kati na hadi Uhindi. Vitawi vya miti hii hutumika kama brashi ya meno na huitwa mswaki pia.