Atbara (mto)

(Elekezwa kutoka Mto Atbarah)

Atbara (kwa Kiarabu: نهر عطبرة, Nahr ʿAṭbara) ni tawimto la Nile linalopatikana kaskazini magharibi mwa Ethiopia na katika Sudan.

Mto wa Atbara
Chanzo Ethiopia, milima ya Simien
Mdomo Nile kwenye mji wa Atbara (Sudan)
Nchi Ethiopia, Sudan
Urefu 800 km
Kimo cha chanzo m
Tawimito mto Tekeze (Setit)
Mkondo hubadilika sana na majira
Eneo la beseni 100,000 km²
Miji mikubwa kando lake Atbara
Ramani ya beseni la mto Atbara.
Ramani ya beseni la mto Atbara.

Chanzo chake ni katika milima ya Simien (Ethiopia) takriban km 50 kaskazini kwa Ziwa Tana au km 30 magharibi kwa mji wa Gondar.

Tawimto lake ni hasa mto Tekeze (Setit) ambao una matawimto mengi. Kiasi cha maji ndani ya Atbara hubadilika sana. Miezi mingi ni mto mdogo sana unaopita katika nchi yabisi lakini wakati wa mvua katika nyanda za juu za Ethiopia unakuwa mpana wenye maji mengi.

Kwenye mji wa Atbara nchini Sudan unaishia katika mto Nile, ukiwa tawimto lake la mwisho kabla ya kufikia Bahari ya Kati.

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Atbara (mto) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.