Mto Sao Francisco (kwa Kireno: São Francisco; kabla ya kufika kwa Wareno wenyeji waliuita Opara) ni mto wa huko Brazil.

Mto Sao Francisco
Beseni ya Mto Sao Francisco
Chanzo Milima ya jimbo la Minas Gerais
Nchi Brazil
Urefu km 2,830
Mkondo kawaida m3/s 2,943, wa chini m3/s 1,480, wa juu m3/s 11,718
Eneo la beseni km2 641,000
Miji mikubwa kando lake [Pirapora]], São Francisco, Januária, Bom Jesus da Lapa,Petrolina na Juazeiro, Paulo Afonso
Mto Sao Francisco, Brazil
Rio Sao Francisco karibu na mdomo wake

Urefu wake ni karibu kilomita 3,100. Matawimto makuu yake ni mito Paropeba, Abaeté, das Velhas, Jequitaí, Paracatu, Urucuia, Verde Grande, Carinhanha, Corrente, na Grande.

Ni mto mrefu kabisa unaopita ndani ya Brazil kuanzia chanzo hadi mdomo, ni mto mrefu wa nne katika Amerika Kusini, baada ya Amazonas, Mto Parana na Mto Madeira.

Jina lilichaguliwa na Amerigo Vespucci aliyekuwa Mzungu wa kwanza kuona mdomo wa mto alipopita huko kwenye 4 Oktoba 1501, sikukuu ya mtakatifu Fransisko wa Assisi katika Kanisa Katoliki.


13°10′33″S 43°25′05″W / 13.17577°S 43.41797°W / -13.17577; -43.41797

Makala hii kuhusu maeneo ya Brazil bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mto Sao Francisco kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.