Mto Turkwel

ni mto unaotoka mlima Elgon mpakani mwa Kenya na Uganda hadi Ziwa Turkana. Mto huu unaitwa Mto Suam kutoka chanzo chake hadi mpakani katika Kaunti ya Turkana nchini Kenya.

Mto Turkwel[1] (pia: Turkwell[2][3]) unapatikana katika kaunti ya Turkana nchini Kenya na unaishia katika ziwa Turkana, lililo kubwa kuliko maziwa yote ya jangwani yaliyoko duniani kote[4].

Mto Turkwel ukiwa umekauka karibu na Lodwar.

Chanzo chake ni katika Mlima Elgon, mpakani mwa Kenya na Uganda na unaitwa kwanza mto Suam. Upande wa kaskazini wa Kapenguria katika kaunti ya West Pokot njia yake imezuiwa na lambo linalounda Bwawa la Turkwel.

Mara nyingi maji yake hayatoshi kufika ziwani na mto unakauka mapema.

Delta ya mto Turkwel Delta inapatikana kwenye mita 369 juu ya usawa wa bahari, mara baada ya kuingia katika kaunti ya Marsabit[5]. 3°06′17″N 36°05′51″E / 3.10472°N 36.09750°E / 3.10472; 36.09750

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  1. Turkwel (Approved) kwenye GEOnet Names Server, United States National Geospatial-Intelligence Agency
  2. Turkwell (Variant) kwenye GEOnet Names Server, United States National Geospatial-Intelligence Agency
  3. The name Turkwel is derived from the Turkana name for the river, Tir-kol, which means translates to a river that "withstands the wilderness"
  4. Adams, W. M. (1989). "Dam construction and the degradation of floodplain forest on the Turkwel River, Kenya". Land Degradation & Development. 1 (3). Wiley: 189–198. doi:10.1002/ldr.3400010303.
  5. Its coordinates are 3°4'0" N and 36°9'0" E in DMS (Degrees Minutes Seconds) or 3.06667 and 36.15 (in decimal degrees). Its UTM position is AD83 and its Joint Operation Graphics reference is NA37-01.

Viungo vya nje

hariri