Kaunti ya Marsabit
Kaunti ya Marsabit ni mojawapo ya kaunti za Kenya zilizopo baada ya katiba mpya ya Jamhuri ya Kenya kupatikana mwaka 2010.
Kaunti ya Marsabit | |||||
---|---|---|---|---|---|
Kaunti | |||||
Makao Makuu ya serikali ya Kaunti ya Marsabit | |||||
| |||||
Marsabit County in Kenya.svg Kaunti ya Marsabit katika Kenya | |||||
Coordinates: 2°19′N 37°58′E / 2.317°N 37.967°E | |||||
Nchi | Kenya | ||||
Namba | 10 | ||||
Ilianzishwa | Tarehe 4 Machi, 2013 | ||||
Ilitanguliwa na | Mkoa wa Mashariki | ||||
Makao Makuu | Marsabit | ||||
Miji mingine | Moyale, Sololo | ||||
Gavana | Mohsmuf Mohamed Ali | ||||
Naibu wa Gavana | Solomon Gubo Riwe | ||||
Seneta | Godana Hargura | ||||
Mbunge Mwanamke(Bunge la Taifa) | Safia Sheikh Adan | ||||
Bunge la Kaunti | Bunge la Kaunti ya Marsabit | ||||
Wawakilishi wa Bunge la Kaunti waliochaguliwa | 20 | ||||
Maeneo bunge/Kaunti ndogo | 4 | ||||
Eneo | km2 70 944.1 (sq mi 27 391.7) | ||||
Idadi ya watu | 459,785 | ||||
Wiani wa idadi ya watu | 6 | ||||
Kanda muda | Saa za Afrika Mashariki (UTC+3) | ||||
Tovuti | marsabit.go.ke |
Wakati wa sensa ya mwaka 2019 wakazi walikuwa 459,785 katika eneo la km2 70,944.1, msongamano ukiwa hivyo wa watu 6 kwa kilometa mraba[1]..
Makao makuu yako Marsabit. Mji mkubwa zaidi ni Moyale ulio katika mpaka wa Kenya na Uhabeshi.
Jiografia
haririKaunti ya marsabit ni kavu. Ina Jangwa la Chalbi ambalo ni jangwa halisi pekee katika Kenya.
Kaunti za Marsabit, Turkana na Samburu hushiriki Ziwa Turkana.
Hifadhi ya Taifa ya Sibiloi hupatikana katika fuo za Ziwa Turkana upande wa Marsabit. Hifadhi ya Taifa ya Losai hupatikana katika mpaka wa Kaunti ya Marsabit na Samburu. Mlima Marsabit uko katika Hifadhi ya Taifa ya Marsabit. Mlima Kulal na Vilima vya Huri hupatikana katika kaunti hii.
Utawala
haririKaunti ya Marsabit imegawanywa maeneo bunge yafuatayo[2]:
Eneo bunge | Kata |
---|---|
Moyale | Butiye, Sololo, Heillu/Manyatta, Golbo, Moyale Mjini, Uran, Obbu |
North Horr | Dukana, Maikona, Turbi, Horr Kaskazini, Illeret |
Saku | Sagate/Jaldesa, Karare, Marsabit ya Kati |
Laisamis | Loiyangalani, Kargi/Horr Kusini, Korr/Ngurunit, Logo Logo, Laisamis |
- Loiyangalani 35,713
- Marsabit Central 79,181
- Marsabit North 54,297
- Marsabit South 65,376
- Moyale 108,949
- North Horr 71,447
- Sololo 44,822
Tazama pia
haririMarejeo
hariri- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-11-13. Iliwekwa mnamo 2021-05-29.
- ↑ "Kuhusu Marsabit Archived 29 Machi 2018 at the Wayback Machine.", Serikali ya Marsabit, ilipatikana 13-04-2018
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-11-13. Iliwekwa mnamo 2021-05-29.
Makala hii kuhusu maeneo ya Kenya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Kaunti ya Marsabit kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |