Archive Hii ni ukurasa wa Hifadhi ya Majadiliano ya Awali. Usihariri ukurasa huu usiongeze wala kupunguza kitu.
Ukitaka kujadiliana upya mambo yaliyomo humo nenda kwa ukurasa wa majadiliano ya sasa.

Karibu

Asante kwa maelekezo yako kuhusu vichwa vidogo vya makala. Nazidi kujifunza kazi yetu hii. Nikikosea mengine mzidi kunielimisha! Nifanyeje kukamilisha kichwa cha makala ya mwisho (niliandika Klara tu, kumbe ingefaa kuandika wazi zaidi Klara wa Asizi) ? User:Riccardo Riccioni

Salam. Siwezi kukujibu vizuri swali lako kwakuwa sikufahamu wewe ni nani!! Tafadhali naomba uweke sahihi yako itakayo saidia kufahamu ni nani aliyekuachia ujumbe katika ukumbi wa majadiliano!! Basi kila lakheri na naomba nijulishe we ni nani?--Mwanaharakati (talk) 04:51, 18 Februari 2008 (UTC)

Good Afternoon Muddyb Blast Producer,

Could you please write a stub http://sw.wikipedia.org/wiki/Auckland_Grammar_School - just a few sentences based on http://en.wikipedia.org/wiki/Auckland_Grammar_School? Only 2-5 sentences enough. Please. --Per Angusta 04:09, 1 Februari 2008 (UTC)

Thanks Muddyb Blast Producer for the superb article!
I have expressed my Support for your Adminship Application. You are a good man. --Per Angusta 08:28, 1 Februari 2008 (UTC)

Kufaulu

1. wauliza kama nimefaulu. Unamaanisha hasa nini? Ukurasa wako nimesharudisha.

2. Ukurasa wa mwanzo ni sawa. Naona ni vema kubadilisha "makala maalumu" wakati mwingine. Ukiona Disney sawa basi uweke. Umebadilisha kingine? --User_talk:Kipala 21:59, 2 Februari 2008 (UTC)

Ukurasa wa mwanzo

Muddy, nakubali kabisa! Nilianza mtindo huu wa kubadilisha lakini nafurahia ukiingia pia. Naona tushirikiane! Pendekezo: Tupange wakati wa Ijumaa. Kama wewe hujabadilisha Ijumaa nitajisikia huru kutafuta kingine. --User_talk:Kipala 18:02, 5 Februari 2008 (UTC)

Picha za Dar

Muddy je utapata nafasi siku moja kuchukua picha kadhaa za Dar? Haina haraka lakini ikiwezekana ningefurahia picha zifuatazo: sanamu ya Askari (njiapanda ya Samora/ Azikiwe=Maktaba - lakini ingekuwa vema kuchagua mwanga vizuri kwa sababu sanamu ni nyeusi; kwa mfano kupiga picha upande wa jua na kuwa na sehemu ya nyuma isiyo mwanga; nadhani kuna uwezekano kupata miti mibichi sehemu ya nyuma); halafu mwandiko wa Kiswahili/Kiarabu kwenye sanamu hii; Halafu moja-mbili kati ya nyumba hizi za kale zilizopo kando la bahari kwa mfano Atiman House (ni nyumba ya White Fathers Sokoine Drive karibu na kanisa St Joseph yaani kati ya Bridge na Mkwepu); palepale Soline Drive ukiendelea kidogo kupitia kanisa la St. Joseph kuna majengo moja mawili ya zamani za Wajerumani pia; halafu soko la samaki pale Kivukoni; halafu picha ya soko la Kariakoo; sijui unazunguka kiasi gani mjini Dar ? Haina haraka kabisa lakini yoyote itakuwa vema. Salaam --User_talk:Kipala 13:07, 9 Februari 2008 (UTC)

Ni sawa, nashukuru sana - kumbuka haina haraka utakapompata rafiki mwenye kamera. --User_talk:Kipala 07:12, 11 Februari 2008 (UTC)


Archive

Muddy naomba usifanye kitu hiki tena. Kweli haifai kuingilia kati katika ukurasa wa mtu mwingine. Mimi binafsi sina hasira niliwahi kuwaza nifanye hivi ila tu kwa utaratibu haitakiwi. --User_talk:Kipala 22:02, 12 Februari 2008 (UTC)

Templeti Muigizaji

Muddy nimeangalia templeti tena haina matata. Kwa hiyo kuna maelezo mawili:

  • ama ni kweli walibadilisha kitu kwenye server kwa hiyo templeti kwa muda haikuwa sawa.
  • au ni tatizo la kompyuta moja-moja wakati wa kuonyesha picha au templeti hii. Nilipotazama masaa 3 yaliyopita nilikaa shule niliona templeti upande wa kushoto na bila mstari wa nje. -- Ikitokea tena ni afadhali kutosema tu "imeharibika" lakini heri kueleza kwa kifupi tofauti ni nini. --User_talk:Kipala 20:10, 13 Februari 2008 (UTC)

Kucheza kwa templeti

Hata mimi naona leo hii kucheza kwa templeti jinsi unavyoona wewe. Aseniki na Ujerumani kama katika sreenshot yako. Hata nchi mbalimbali. Lakini mimea ya ChriKo ni sawa. Sijui ni nini inawezekana kitu fulani kinacheza. BAsi hakuna cha kufanya ila kutulia, kusubiri na kuitazama. --User_talk:Kipala 07:27, 15 Februari 2008 (UTC)

Najaribu kupata ushauri tazama http://meta.wikimedia.org/wiki/User_talk:Pathoschild#Advice_on_formats. --User_talk:Kipala 11:22, 19 Februari 2008 (UTC)

haki za mkabidhi

Pole sana. Sijagundua jinsi ya kufanya kazi za bureaucrat. Pia inawezekana kuwa sija tambuliwa na shirika la wikipedia, yaani sijapewa haki ya kufanya kazi hizo. Pia kampuni linalonipa kuingia mtandaoni (internet provider) lina shida nyingi sana. Nimebanwa kabisa. Pole tena! --Oliver Stegen 07:33, 1 Machi 2008 (UTC)

Haya nimejitahidi kujifunza haraka. Umepata haki za mkabidhi sasa. Hongera! Tukazane na kazi njema. --Oliver Stegen 09:01, 1 Machi 2008 (UTC)

Uteuzi mpya

Kuna pendekezo jipya kwa bureaucrat. Naomba uangalie ukurasa wa wakabidhi. --Oliver Stegen 09:14, 1 Machi 2008 (UTC)

Makala za msingi

Muddy salaam. Ukiendelea kutumia ujuzi wako katika muziki na watu wa filamu labda angalia [1]. Ni orodha ya makala za kimsingi kutoka meta:wiki (meta ni wiki kwa ajili ya mradi wote wa wikipedia ya kila lugha). Ni mapendekezo tu lakini inaangaliwa katika takwimu ya Meta pale penye kulinganisha wikipedia mbalimbali. Udhaifu ni ya kwamba mtazamo wa orodha ni ya Kimarekani kabisa. Isipokuwa sioni ya kwamba orodha ya makala za msingi za kamusi elezo kwetu sw:wiki ni afadhali kwa sababu inakosa mpangilio mwema. Mimi nimeamua kutunga makala angalau fupi zinazofuata orodha ile ya meta. Mfano kwa takwimu: Yoruba imetupita sasa katika idadi ya makala - lakini ukiingia ndani ni hewa tu yaani makala nyingi za sentensi moja basi zinatenengenezwa kwa kutumia bot yaani programu inayotafsiri. Linganisha Abuja kwao na kwetu. Hata mibegu mifupi kwetu afadhali. Hii ni sababu ya kwamba katika orodha nyingine ya meta:List of Wikipedias by sample of articles wako chini kabisa. Hivyo napendekeza kukaza kidogo orodha hii inayotuongezea sifa. --User_talk:Kipala 17:17, 2 Machi 2008 (UTC)

DEFAULTSORT:...

Kuhusu swali lako la kuingiza DEFAULTSORT: "jina la familia", "jina la kwanza" kwenye makala ya mtu, maana yake ni kuorodhesha watu katika jamii fulani. Kwa mfano, ukiangalia Category:Wanamuziki wa Marekani, wanamuziki wote wameorodheshwa kufuatana na majina yao. Bila DEFAULTSORT, Stevie Wonder angeonekana chini ya S, lakini pamoja na format hii (yaani DEF: Wonder, S), atatajwa chini ya W. Asante kwa swali lako. Endelea kuuliza. Nakutakia kazi njema. --Oliver Stegen 12:25, 5 Machi 2008 (UTC)

Pendekezo la jalada

Asante kwa kuniheshimu na kuweka jalada zangu za majadiliano ya zamani kama mfano kwenye sanduku la mchanga. Naona ni vema tu. Hongera kwa kazi bora! Wasalaam, --Oliver Stegen 09:14, 8 Machi 2008 (UTC)

pakia faili??

Muddy, kwanza nashukuru kwa salamu na hongera za bureaucrat. Sasa niandike kingine nimeona tatizo sijui nimwulize nani. Hii "pakia" faili" kwa upload ya picha imebadilika haifanyi kazi tena. Sijui kama wakati wa kushughulika vitufe umegusa sehemu hiyo? Naomba angalia faili ya Wikipedia:Upload inaonekana ama imepotea au kiungo chake. Asante --User_talk:Kipala (majadiliano) 13:46, 13 Machi 2008 (UTC)

Kiwashio

Muddy, salaam naomba unisaidie lugha. Nimetumia "kiwashio" lakini sina uhakika inaeleweka jinsi gani. Naelewa ni "kifaa cha kuwasha". Niliitumia kwa sehemu ya ramia yenye dawa kali ndani yake inayopigwa na msumari wa bunduki na kuwaka ikiwasha baruti. Sasa naona hutumiwa pia kwa "swichi" ya umeme yaani kifaa kinachowasha taa. (nilikaa muda mrefu Kneya huku watumia "swichi" tu). Je kwa ramia na baruti inaeleweka au hapana? --User_talk:Kipala (majadiliano) 14:14, 19 Machi 2008 (UTC)

Bombomu

Muddy salaam nahitaji tena usaidizi wa lugha. A) Je nimeelewa vema hapo juu ya kwamba "kiwashio" ni sawa pia kwa kidude kinachowasha ramia?

B) Bombomu (machine gun): kamusi zote zina maneno kadhaa lakini sina uhakika kama chaguo langu ni sawa. Nimeona sasa "bombomu" hutumiwa pia kwa "bomu" (bomb). Chaguo nyingine ilikuwa "bunduki ya mtombo". Ipi afadhali? --User_talk:Kipala (majadiliano) 16:02, 19 Machi 2008 (UTC)

Neno ninalohitaji ni ya "machine gun" - lipi? Bombomu, "bunduki ya mtombo" au nini? --User_talk:Kipala (majadiliano) 16:09, 19 Machi 2008 (UTC)
Sub machine gun - sawa. Menginevyo: nategemea mara nyingi kamusi na pale ambako hazieleweki nakaa gizani. Hata watu wa TUKI kwenu Dar mara kadhaaa wameandika kitu ambacho hakuwezekani. Basi nitahamisha yote kwa "bunduki ya mtombo" nitafuata ushauri wako. --User_talk:Kipala (majadiliano) 16:20, 19 Machi 2008 (UTC)


Basi heri ya sikukuu!--User_talk:Kipala (majadiliano) 16:36, 19 Machi 2008 (UTC)

Sofia Rotaru

Hello, could oyu please help to translate at least introduction of the article on Sofia Rotaru, from English or Russian Wikipedia (which is best for you). I could help you with an article of your choice in Russian, Romanian or English. Thank you very much in advance.--Milesgive (majadiliano) 20:38, 25 Machi 2008 (UTC)

Templeti Mchezaji

We babu Shikamoo. Maana toka uwe mkabidhi umeasimika na huonekani kama milango ya baiskeli. Dawa yako Tanesco tu! We jidai upo bize. Sasa ungefanya mpango wa Templeti husika hapo juu aidha iwe templeti mchezaji mpira, mchezaji mpira wa miguu, mcheza soka au vyovyote itakavyo kukalia sawa. Ukiona namna gani vipi ipindue ile ya kwenye en uilete kwenye sw wiki. Muda mrefu nafukuzia hilo ila nadhani wakati wake dio huu. Kazi njema. Shemeji! 12:35, 26 Machi 2008 (UTC)

Mzungu na interwiki

Muddy, makala ya "mzungu" nimeongeza kidogo nadhani nimepata ufumbuzi baada ya kuchimba kwenye kamusi (usidharau kamusi tena!).

Halafu ombi: Naona unafuatilia sana wale wanamuziki kutoka orodha ya Meta. Nashukuru. Kwa kuonekana katika takwimu ya List_of_Wikipedias_by_sample_of_articles inasaidia kuziingiza pia katika makala ya en:wiki. Maana ile takwimu inapitia interwiki za en:wiki tu kwa hesabu yake. Nimejaribu kuifanya kwa makala zote bila shaka kuna chache ambazo sijapata bado. Nimegundua kama si sisi tunaoingiza makala zetu katika interwiki ya en:wiki basi tunabahatika kama bot fulani inakuta makala zetu na kuziandika. basi ni haya tu, likizo zangu zinakwisha sitaonekana tena mara nyingi jinsi ilivyokuwa. --78.49.199.167 09:49, 26 Machi 2008 (UTC)

Hongera ya kukamilisha mwaka!

Muddy napenda kukupa hongera kwa kukamilisha mwaka kwenye wikipedia hii yetu. Nataka pia kusema asante kwa ushirikiano mwema na kazi nzuri! Ubarikiwe! --Kipala (majadiliano) 09:43, 2 Aprili 2008 (UTC)

Vyakula

Muddy naomba chungulia makala ya vyakula hasa mboga na jamii kunde. Nimeyaandika kwa kumaliza ile orodha sina uhakika kama niko sawa. Jamii kunde ni lugha ya kamusi sijui kama inaeleweka. Mboga ninavyojumlisha ni zaidi kutafsiri sina uhakika matumizi hali halisi ni yapi. --Kipala (majadiliano) 10:29, 5 Aprili 2008 (UTC)

Mwanzo

Pole na matata, kwangu kila kitu sawa angalia picha ya sasa hivi

 
Mwanzo kwangu leo hii

--Kipala (majadiliano) 15:15, 16 Aprili 2008 (UTC)

Kwangu hakuna mpolisi. --Kipala (majadiliano) 15:35, 16 Aprili 2008 (UTC)
Pole sana sijui. Sidhani sana kama hii ni kitu kutoka intaneti ingawa landa ni aina ya virusi (kama haileta hasara zaidi basi). Sijui kama ofisi imeweka programu kwenye tarakilishi inayoonya kama kurasa zisizo za kazi zinatembelewa?? Lakini kama ni programu kama hiyo itaonekana pia kuiangalia kurasa nyinginbe. Isiposumbua zaidi usijali na subiri kama iko tena kesho. --Kipala (majadiliano) 15:54, 16 Aprili 2008 (UTC)
Je imeruditena leo hii? --Kipala (majadiliano) 07:56, 17 Aprili 2008 (UTC)

Kinanda

Salamu pole na polisi lakini kama si programu ya mwajiri wako ya kukuambia "Usipoteze muda wako kwa kucheza" basi uichukue kama jini mwema atakayekulinda.

Kinanda nilitaka kuuliza. Naomba ufanye upelelezi kidogo. Naona katika kamusi zangu ya kwamba kiasili ilikuwa jina kwa kila ala ya muziki yenye waya (kama banjo, gitaa, n.k.). Halafu jina limepanuka kutaja pia "piano" (ina pia nyaya ndani yake kwa sauti) lakini baadaye pia ala zote zinazofanana na piano kama ogani na hizi keyboard. (hivyo kamusi ya Bakhressa pia M-J SSE) Lakini TUKI-ESD na TUKI-SED zina pia maneno kama ogani, piano, nusu kinanda.

Sasa sijui matumizi hali halisi. Bado ala ya kufanana na banjo/gitaa ni "kinanda"? Watu wa bendi wasiposema "keyboard" wanasemaje? Hii piano ikionekana kwenye picha inaitwaje? Naomba uwaulize wazee na pia vijana kadhaa, Waswahili pamoja na watu wa bara. Asante --Kipala (majadiliano) 07:57, 18 Aprili 2008 (UTC)

7000

Muddy, asante kwa salamu. Kweli 7,000 ni namba nzuri. Sasa nasikia 10,000 inakaribia. Isipokuwa nikikumbuka ilikuwa kazi gani kutoka 4000 hadi hapa nasikia uchovu kidogo. Lakini tutaendelea tu.Safari nilishangaa jinsi tulivyoruka kutoka 5000 hadi hapa tangu Julai 2007 - jamani. Nimepata hoja sijui unaonaje. Nikijaribu kupata nakala ya CD ya wikipedia yetu jinsi ilivyo - inaweza kusaidia kuvuta watu wakipata nafasi kuchungulia harakaharaka bila kusubiri nyavu? --Kipala (majadiliano) 17:35, 21 Aprili 2008 (UTC)

Hongera kwako! Labda hadi 5000 nilichangia kiasi ila sasa ni wewe uliyeanza kuchangia zaidi. Nakufurahia na kukushukuru na kusema tena: Hongera! --Baba Tabita (majadiliano) 09:04, 25 Aprili 2008 (UTC)

Jamii

Muddy, salaam. Nimekumbuka tatizo moja nililokuwa nalo naona na wewe umelipata. Kuunda jamii inaleta kazi ya kupanga jamii. Yaani ukiunda makala za wasanii (kwa mfano) je jamii zake zinaunganishwa wapi? Mfano: Sofia Rotaru umempangia jamii ya "Wanamuziki wa Ukraine". Jamii hii imebaki wa rangi ya rangi nyekundu kwa sababu iko pekee yake. Njia nzuri ni ni kuunganisha jamii ya "Wanamuziki wa Ukraine" na A) jamii:watu wa Ukraine na B) Wanamuziki (labda nchi kwa nchi). Unaonaje ? --Kipala (majadiliano) 23:31, 30 Aprili 2008 (UTC)

A little help: Ecser

Salaam, jambo! I'm a Hungarian Wikipedia editor, my name is Norbert Kiss. I'm very proud of my village and I would like to read about it in a lot of langauges. I translated already it into 10 languages (now it is in 28 languages), but I can't speak kiSwahili. Could you help me? My village's English page is this: Ecser. Could you translate the page of Ecser into kiSwahili? Then just link the side into the English version and I will see it, or you could write me, when it is ready. My Hungarian Wikipedia side is: My profile.

Thank you! Norbert

Thank you

Thank you for you translation-help. I know, that it is not so important to have an article about an unknown hungarian village, but in my soul it is very important to me. And the kiSwahili is one of the greatest languages of Africa. I have home a Swahili text book, I tried to translate it with the help of that. I will try to do some other interesting articles about Hungary. We, Hungarians did and do a lot of things for Africa. You can find a volcano called Teleki somewhere in Kenya or Tanzania (I don't remember well), it is named after a Hungarian explorer. Or a missionary, István Czimerman created the writing of the Nyungwe language in Mozambique. Ot László Magyar, who became a leader of a tribe in Angola. We love Afica! :)

- Norbert

Map

Could you upload this map to Swahili Wikipedia? Map of the place of the Hungarian language in the Carpathian basin... I would like to use it in the Kihungaria page. - --Eino81 (majadiliano) 09:54, 20 Mei 2008 (UTC)

Ok, I understand. Thank you :) - --Eino81 (majadiliano) 10:26, 20 Mei 2008 (UTC)
But look, now I put an other map to the same side, with your method, but it still not work. sometimes an administrator must to upload these pictures. When I tried to edit in other Wikipages, the situation was the same. It is common, in the Wikipeida, but not in every langauges... Kihungaria. ---Eino81 (majadiliano) 10:35, 20 Mei 2008 (UTC)
this one: Kifini-Kugori
Thank you. Excuse me for the everytime disturbation, but in the Hungarian Wikipedia everyone can upload a file... - --Eino81 (majadiliano) 13:20, 20 Mei 2008 (UTC)
But as you see, the Kihungaria page is greater and greater :) - The Swahili Wikipedia is growing :) - --Eino81 (majadiliano) 13:45, 20 Mei 2008 (UTC)


Help

Please, coul you translate this article onto Swahili, please? A stub is enough. If you want to translate any article onto Spanish, Catalonian or Galician, tell it to me please. Chabi

It's already exiest. See: Kitabu cha Mormoni. Your welcome!--Mwanaharakati (majadiliano) 05:14, 2 Juni 2008 (UTC)
Thanks a lot. If you wanna translate any article on those languages, tell it to me, please. --85.54.140.245 12:56, 2 Juni 2008 (UTC)

dau-mdau[wadau

Muddy, naomba nisaidie kuelewa vema lugha hii ya kuita watu dau --mdau- wadau. Inamaanisha nini? Asante --Kipala (majadiliano) 14:51, 4 Juni 2008 (UTC)

Maelekezo

Ndugu, nashukuru kwa maelekezo yote uliyonipatia hata leo na kwa yale utakayoendelea kunipatia ili kuboresha wiki. Usichoke kwa kuwa yanahitajika. Kuhusu kufuta ile picha, subiri kwanza uone kama hapa nimefaulu kutekeleza au bado... Riccardo Riccioni--Riccardo Riccioni (majadiliano) 10:20, 13 Juni 2008 (UTC)

action concept

action concept Film- und Stuntproduktion GmbH ni kampuni ya filamu nchini Ujerumani. Inashughulika hasa mambo ya STUNT na ACTION. Kampuni ilianzishwa 1992 ikiwa na waajiriwa 150 na biashara ya Euro milioni 40 kwa mwaka. Ilijipatia sifa kwa ajili ya STUNT katika filamu za TV ya Kijerumani. 2003 kampuni ilipewa tuzo la World Stunt Award kwa kazi yake katika filamu za SERIES „Wild Angels“ kwa „STUNT bora ya filamu isiyo ya Kiingereza“. Ilipata pia Taurus Awards kwenye miaka ya 2004, 2005 und 2007. Kampuni inafundisha waigizaji wa STUNT ikiendesha kozi zake yenyewe.

(eti STUNT sina neno sijui utafanyaje?)

Changamoto - mwanafunzi wa mwisho

Ni filamu ya kampuni action concept Film- und Stuntproduktion GmbH ya mwaka 2005.

Hadithi

Baada ya kipindi cha matatanisho ya kiuchumi Ulaya ingia katika hali ya vita ya wenyewe kwa wenyewe. Ustaarabu unaharibika kabisa pamoja na miji, viwanda na utamaduni. Lakini katika vurugo mfalme wa majeshi –asiyetajwa kwa jina- anafumbua siri ya sanaa ya kale ya vita anajenga jeshi. Lakini hafikii kwenye ngazi ya juu ya sanaa ile kwa sababu walimu wazee wanakataa kumweleza zaidi. Hapa anaamua kuwaua wote. Walimu wazee wanaandika ujuzi wao katika kitabu kinachokuwa sasa lengo la juhudi za mfalme wa majeshi. Akikutana na mwalimu mzee wa mwisho anauawa naye katika mapigano. Watoto wa mfalme wanaendeleza utawala wake wakiendelea kutafuta kitabu chenye siri ya vita. Miaka kadhaa baadaye Jonas Klingenberg ni mwanafunzi wa pekee wa mwalimu mzee wa mwisho. Huyu anauawa na watoto wa mfalme Bosco na Kleo wanaoiba kitabu chake. Jonas anajeruhiwa vibaya nao wanamwacha wakiamini amekufa. Baada ya kupona Jonas anaona wajibu wake kumzika mwalimu mzee halafu kulipiza kisasi. Anakusanya kundi la wanaume walio tayari kuunga mkono naye. Bosco akiwa na kitabu anajaribu sasa kumkamata Jonas anafaulu kwa njia ya uhaini kumshika rafiki yake Vincent. Jonas anamkomboa Vincent lakini kwenye nafasi hii dada yake Vincent ashikwa. Wakijaribu kumkomboa huyu dada kuna mapigano kati ya Joans na Bosco. Jonas anamshinda ikionekana ya kwamba Bosco hajaelewa wala kitabu wala sanaa ya vita kinyume cha Jonas amabye ni mwanafunzi wa mwisho wa mwalimu mzee. --Kipala (majadiliano) 13:10, 23 Juni 2008 (UTC)

Help needed

Hi Muddyb Blast Producer,

I have left a message on your English talk page. I hope you can help me. --Jose77 (majadiliano) 06:34, 24 Juni 2008 (UTC)

Mwenzako

Muddy, huyu ni idara yako! User_talk:Kipala#Re: Karibu - Naomba umsaidie! --Kipala (majadiliano) 13:35, 7 Julai 2008 (UTC)

Kinanda

Asante sana Muddyb! Niligeuza kurasa wangu. Moongateclimber (majadiliano) 06:37, 8 Julai 2008 (UTC)

mmmmmhhhh.... ninasema kiswahili kidogo tu; your kiswahili is too much for me at the moment (although I thank you for trying). I can guess you're saying something about an infobox/template for song (nyimbo) entries, but I'm not sure what it is exactly. I'm sorry... can you try that in english? :-( Moongateclimber (majadiliano) 12:38, 8 Julai 2008 (UTC)
Asante sana. Wewe ni adili: mimi ni hapa kujifunza. Nitajaribu kusema Kiswahili :-) And forget any mistakes... I will try to keep them in my talk and not in kurasa... Thanks for caring... Moongateclimber (majadiliano) 15:41, 8 Julai 2008 (UTC)

Bendi za musiki nchi kwa nchi

Nilifanya jamii Category:Bendi za muziki wa Tanzania, Category:Bendi za muziki wa Uingereza, pia Category:Bendi za muziki nchi kwa nchi (kama Category:Wanamuziki nchi kwa nchi). Ninatumaini nilifahamu ujumbe wako :-) ~ Moongateclimber (majadiliano)

90125

Asante, ninaonea huruma hatia katika 90125. Juu ya jamii na alama nyekundu: je, Albamu msanii kwa msanii, Albamu mwaka kwa mwaka ni kiswahili adili? (would those be correct titles in Swahili? Albums by artist, Albums by year) Na Albamu studio kwa studio, Albamu mtayarishaji kwa mtayarishaji? Asante Moongateclimber (majadiliano) 06:47, 10 Julai 2008 (UTC)

Angalia

Muddy, naomba uangalie barua pepe zako. --Kipala (majadiliano) 15:12, 15 Julai 2008 (UTC)

Translation request

The translation request
Hi! Could I ask you to translate the article which you can find below into Swahili? Please help me to show our language to the world – the article is quite short and has been selected from English and Silesian article and shortened as possible to contain only the basic informations. If you would finish, please, make me know on my Silesian or Polish discussion. Thanks in advance.
PS. If you want me to translate any article into Polish or Silesian, contact me without hesistation.
So, here’s the text to translation:

The Silesian language (Silesian: ślůnsko godka, ślůnski, sometimes also pů našymu) is a language spoken by people in the Upper Silesia region in Poland, but also in Czech Republic and Germany. In 2002 about 56 000 declared Silesian as their native language, but the number of speakers is estimated on 1 250 000.

Silesian is closely related to Polish language, that’s why it is considered as a dialect of Polish by some linguistics.

Alphabet

There’s not one Silesian alphabet. The Silesian speakers are used to write their language with the Polish characters. In 2006 was invented the new Silesian alphabet, based on all of the Silesian scripts (there’s 10 of them). It is widely used on the Internet, as well as in the Silesian Wikipedia.

Aa Bb Cc Ćć Čč Dd Ee Ff Gg Hh Ii Jj Kk Ll Mm Nn Ńń Oo Pp Rr Řř Ss Śś Šš Tt Uu Ůů Ww Yy Zz Źź Žž

And some digraphs: Ch Dz Dź Dž.

Thank you once again, Timpul (majadiliano) 09:55, 23 Julai 2008 (UTC)

Thank you for your excellent translation :) Really nice language :D Greetings from Poland! Timpul (majadiliano) 17:15, 23 Julai 2008 (UTC)

Ndiyo na hapana...

Nilikuwa na kazi nyingi... Lakini ninalinda hapa mara nyingi. Asante na tutaonana MuddyB! Moongateclimber (majadiliano) 09:50, 24 Julai 2008 (UTC)

Muziki wa Tanzania

Ndiyo, kwa mfano DCC Mlimani Park Orchestra na Orchestra Maquis Original? Katika Wikipedia ya Kiitaliano niliandika kurasa nyingi kuhusu muziki wa Tanzania (bongo flava, muziki wa dansi) na pia muziki wa Afrika. Mimi ninapenda sana muziki wa Afrika! Kwa mfano, husikia bendi nyingi kutoka Kongo (soukous) na Afrika Kusini. Lakini albamu hizi ni zagumu kupata katika Italia! :-) Moongateclimber (majadiliano) 08:30, 25 Julai 2008 (UTC)

P.S. I know kuishi but couldn't find ulishawai on any dictionary. I never lived in Tanzania if that's what you're asking... (otherwise I would probably know some swahili) I visited there a few years ago as a tourist. I'm planning to come back very soon... :-) Moongateclimber (majadiliano) 08:33, 25 Julai 2008 (UTC)

Jamii Wanasoka

As Salaam Alaykum Babu, Kwanza nawaomba mniwie radhi kwa kimya kirefu kidogo kutokana na mambo ya masomo kuwa magumu kiasi. Muddy, naomba unifanyie msaada wa kutengeneza jamii au category kama nitakuwa sahihi ya wanasoka au kama kuna ulazima basi nifundishe kuiumba mwenyewe. (SideMontero)

Re from Thai Wikipedia:

It's ok to me. You can use that template on Kiswahili Wikipedia or Wiktionary if you like. But do remember that some parts are designed for Thai Wikipedia only. You maybe want to change that template a little bit if you want to.

If you want to get help from me, you can ask me for anytime. Also remember that most Thai templates are easier than the English one. We don't want things too complicated.

I must really ask you - what's your English level? Is this English too easy or okay? You want it to be harder or just this?

Goodbye.

--125.24.95.165 10:30, 29 Julai 2008 (UTC)