Munukero (kundinyota)
Munukero (kwa Kilatini na Kiingereza Monoceros) [1] ni jina la kundinyota kwenye nusutufe ya kusini ya dunia yetu.
Mahali pakeEdit
Munukero lipo karibu na ikweta ya anga na katika kanda ya Njia Nyeupe.
Linapakana na makundinyota Shuja (Hydra) upande wa kaskazini, Mbwa Mdogo (Canis Minor), Jauza (Gemini), Jabari (Orion), Arinabu (Lepus), Mbwa Mkubwa ( Canis Maior) na Shetri (Puppis).
JinaEdit
Munukero ni kati ya makundinyota yaliyobobuniwa tangu mabaharia Wazungu walizunguka dunia yote yaani karne ya 16 na hapo wanaastronomia wa Ulaya walilenga kuchora ramani ya nyota zote. Wagiriki wa Kale hawakujaribu kupanga nyota zake hafifu kati ya makundinyota waliyojua.
Mwisho wa karne ya 16 Mholanzi Petrus Plancius alipokea taarifa ya mabaharia waliochora nyota za kusini halafu akajitahidi kujaza eneo lote la angani kwa kupanga nyota zote kwa kundinyota. Hapo alitambua mapengo (yaani nyota zisizopangiwa kwa kundinyota) akaunda maundinyota ya Munukero na Twiga (Camelopardalis) na kuichora katika globu ya nyota yake.
Plancius alitumia jina la Munukero (monoceros) ambayo katika mitholojia ya Ulaya ni mnyama visasili anayefanana na farasi mwenye pembe moja kichwani. Inaaminiwa ya kwamba wazo hili lilitokana na taarifa kuhusu kifaru zilizopokelewa Ulaya. Jina la Kigirkiki la “Monocero” lina sehemu mbili za “mono” yaani moja na Cero yaani pembe.
Leo Munukero - Monoceros iko pia kati orodha ya makundinyota 88 ya Umoja wa Kimataifa wa Astronomia zinazoorodheshwa na Umoja wa kimataifa wa astronomia [2]. Kifupi chake rasmi kufuatana na Ukia ni 'Mon'.[3]
NyotaEdit
Monucero ina nyota chache na dhaifu tu. Nyota angavu zaidi ni α Alfa Monocerotis yenye mwangaza unaoonekana wa mag 3.93 ikiwa umbali wa Dunia miaka nuru 148 [4]