Muskat
(Elekezwa kutoka Muskat, Omani)
Kwa maana nyingine, tazama Muskat (maana).
Maskat (Kiarabu: مسقط) ni mji mkuu pia mji mkubwa wa Omani. Mji una takriban wakazi 650,000.
Jiji la Muskat | |
Mahali pa mji wa Muskat katika Omani |
|
Majiranukta: 23°36′31″N 58°35′31″E / 23.60861°N 58.59194°E | |
Nchi | Omani |
---|---|
Mkoa | Maskat |
Maskat ina historia ndefu. Tangu karne ya 2 ulijulikana kama bandari ya biashara ya kimataifa hasa ya uvumba.
Mwaka 1507 ulivamiwa na Wareno waliokaa hadi kufukuzwa mwaka 1649 na Sultani bin Saif. Baadaye mji ulishambuliwa na Waajemi pia na Waarabu Wahabiyya lakini Sultani Sayyid Said alifaulu kutetea utawala wake. Sayyid Said alihamisha baadaye mji mkuu wake kwenda Zanzibar. Tangu wakati huo mji ulirudi nyuma.
Serikali ya Sultani Qaboos bin Said iliweza kuboresha maisha ya wananchi tangu mwaka 1970 hasa kutokana na mapato ya mafuta ya petroli. Mji wa Maskat ulianza kukua na kupanuka sana.
Viungo vya nje
haririMakala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Muskat kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |