Muundi
Muundi (pia: ugoko; kwa Kilatini na Kiingereza: tibia) ni mfupa mkubwa wa mbele wa mguu ambao unaanzia kifundo hadi goti na umeunganika na mfupa mwingine mdogo ambao umejishikiza kwa sehemu ya pembeni.
Mfupa huo mkubwa huunganika na mfupa mkubwa wa juu pamoja na tishu laini kuunda ungio la goti ambalo ndilo linalobeba uzito mkubwa wa mwili.
Upande wa mbele umefunikwa sanasana na ngozi, mbali ya mafuta machache na mishilio ya tishu laini ya misuli iliyo kama kitambaa. Umbile hilo linafanya kuwe na hatari ya kupata majeraha kwa urahisi kwa sababu ya uchache wa misuli na mafuta ambavyo hutoa ulinzi mkubwa katika maeneo mengi ya mwili kwa kukinga mifupa isifikiwe endapo kitu kitagonga eneo husika.
Upande wa nyuma umefunikwa na misuli ambayo huitwa kigimbi kutokana na kujaa vizuri na hivyo kuzuia urahisi wa kupata majeraha.
Makala hii kuhusu mambo ya anatomia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Muundi kama matumizi yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |