Mwaka Elfu Mbili lilikuwa jina lililotolewa kwa ajili ya tamasha lililofanyika mnamo tarehe 9 Mei, 1999 huko jijini Dar es Salaam, Tanzania. Tamasha hili liliandaliwa na Madunia Foundation na kudhaminiwa na Salama Condoms na msaada wa taarifa zinazopatikana katika wavuti ya Rumba Kali wakati huo (sasa African Hip Hop.com). Dhumuni la kufanya onesho hili ilikuwa kuandaa vipande vya filamu kwa ajili ya dokumentari ya "Hali Halisi. [1] Tamasha lilifanyika katika ukumbi wa FM Club Kinondoni.

Tangazo la tamasha juu ya Mwaka Elfu Mbili.
Huko Salamander: maemcee kutoka Dar, wakiwa na muandaaji mkuu wa tamasha Nd. Ben Hewett aliyesimama kulia kaegemea ukuta. Katikati aliyechutama Imam Abbas kulia na kushoto yake ni KR Mullah.

Wazo kuu linatoka kwa Martin Meulenberg (ambaye ndiye aliyeongoza utengenezwaji wa filamu ya Hali Halisi) na ndiye aliyependekeza kuandaa onesho hili kwa nia ya kukusanya maoni mbalimbali kutoka kwa wasanii tofauti. Kwa kutumia taarifa zilizokusanywa na mtandao wa Rumba Kali, ilikuwa rahisi kutengeneza vipeperushi vinavyotoa taarifa sahihi kuhusu onesho hili. Wakati wa onesho walifanikiwa kufanya mahojiano na wasanii zaidi ya ishirini kisha baadaye wakaenda Arusha na Zanzibar.

Gangwe Mobb upande wa kushoto (Inspector Haroun kainamia meza anaandika) na wa mbele yake Dogo Side, na G.W.M. upande wa kulia (D-Chief kushoto na KR Mullah kulia).

Baadhi ya wasanii walionekana kwenye posta ya tamasha hili ni pamoja na Gangwe Mobb, Deplowmatz, G.W.M, Unique Sisters, II Proud, KBC (Kwanza Unit, Underground Souls, X Plastaz, Fortune Tellers na wasanii wengine ambao walitangazwa katika redio ya Clouds kipindi ndiyo inaanzishwa. Wakati huu KBC alikuwa mtangazaji katika kipindi cha kila wiki cha "Underground Hip Hop Show".[2]

Tamasha hili ndio kali haliwajawahi kutokea kwa kipindi hicho tangu hip hop ya Tanzania ianze. Sehemu kubwa ya wasanii wakubwa kwa kipindi kile walishiriki. Hata wale walioalikwa baadhi yao walishindwa kutumbuizwa hasa kwa kutokana na muda na vilevile mwamko ulikuwa mkubwa sana. KBC na Bonny Luv huko Clouds FM karibia wiki nzima walikuwa wanaalika marapa katika kipindi chao ili kuchochea onesho hili.

Tazama pia hariri

Marejeo hariri