Mwezi mwandamo
Mwezi mwandamo ni awamu ya Mwezi ambako hauonekani kwa macho. Awamu hili linatokea kila baada ya siku 29 1/2.

Awamu za mwezi kuanzia mwezi mwandamo (1) kupitia hilali (2), robo ya kwanza, nusu mwezi, robo ya tatu, mwezi mpevu (5) hadi mwezi mwandamo tena
Katika awamu hii Mwezi uko kati ya Dunia na Jua. Hivyo ni nusu ya Mwezi isiyoonekana kutoka Duniani inayopokea nuru ya Jua lakini upande ambao tunatazama uko kivulini.
Hali halisi upande unaotazama Dunia hauko gizani kabisa kwa sababu unapokea kiasi cha nuru inayoakisiwa kutoka uso wa Dunia.