Nacer Barazite (alizaliwa Nijmegen, Uholanzi, 27 Mei 1990) ni mchezaji wa kandanda wa Uholanzi mwenye asili ya Moroko. Anaweza kucheza kama mchezaji wa kati ya uwanja anayeshambulia ama kama mshambulizi msaidizi.

Nacer Barazite
Maelezo binafsi
Jina kamili Nacer Barazite
Tarehe ya kuzaliwa 27 Mei 1990
Mahala pa kuzaliwa    Nijmegen, Uholanzi
Urefu 1.88m
Nafasi anayochezea Mshambulizi
Maelezo ya klabu
Klabu ya sasa Arsenal
Namba 33
Klabu za vijana
Monaco Arsenal,
Klabu za ukubwani
Miaka Klabu
Derby County katika mpango wa mkopo
Timu ya taifa
Uholanzi ya vijana walio chini wa umri wa miaka 19

* Magoli alioshinda

Wasifu wa Klabu

hariri

Barazite alianza kucheza kama kijana katika klabu ya mji wake wa kinyumbani, NEC. Alijiunga na Arsenal katika mwaka wa 2006 na mara kwa mara amehusika katika mechi ya timu hifadhi na timu ya vijana chini ya umri wa miaka 18 katika msimu wa 20006-07. Yeye alitia saini mkataba maalum na klabu hii mnamo Septemba 2007, akiwa amefunga akiwa timu ya kwanza katika mechi za kirafiki dhidi ya Barnet, mwezi uliopita.

Barazite alichezea timu ya kwanza katika mechi ya kushindana kwa mara ya kwanza 31 Oktoba 2007.Aliingi kama mchezaji mbadala kwa Eduardo da Silva dhidi ya Sheffield United katika mechi ya Shindano la Kombe la League. Mechi yake ,akiwa timu ya kwanza, ya pili aliingia kama mbadala wa Mark Randall katika Shindano la Kombe la League katika robo fainali dhidi ya Blackburn Rovers mnamo 18 Desemba 2007. Ingawaje,dakika 17 baada ya kuingia uwanjani alitolewa kutoka mechi akiwa na bega limeumia na akabadilishwa na Fran Merida.

Barazite akarudi kuchezea timu hifadhi baada ya jeraha lake,alifunga mabao matatu akiwa timu ya vijana wa chini ya umri wa miaka 18 wa timu ya Arsenal wakishinda Southampton 5-2. Mabao mengine mawili yalifungwa na Luke Freeman. Barazite pia alikuwa miongoni mwa wachezaji wabadala wa Arsenal katika mechi ya mwisho ya ligi dhidi ya Sunderland hapo 11 Mei 2008,lakini hakucheza.

Barazite alihusika katika kampeni ya kabla ya msimu wa 2008-09,akafunga bao la Arsenal wakashinda 2-1 dhidi ya Barnet katika mechi ya kirafiki huko Underhill mwezi wa Julai. Tarehe 19 Agosti 2008, Barazite alijiunga na timu ya Derby County,hapo awali mkataba ulikuwa hadi mwisho wa mwaka lakini aliongeza ifike mwisho wa msimu. Barazite alipewa taji la Mchezaji bora wa Mechi ,Derby iliposhinda mechi yao ya kwanza baada ya karibu mwaka mmoja bila ushindi,Barazite aliingia baada ya dakika 45. Yeye alikuwa muhimu katika ushindi wao wa 2-1 alipowasaidia na kumpa mchezaji mpira na akafunga katika dakika za mwisho wa mechi. Tarehe 29 Desemba 2008, alithibitisha kwamba mkataba wa mkopo wake ungeendelea na Derby County hadi mwisho wa msimu wa 2008-09. Yeye alifunga bao lake la kwanza kwa timu ya Derby 18 Februari dhidi ya Blackpool.

Msimu wa 2009/10

hariri

Barazite alicheza katika michuano ya kampeni ya kabla ya msimu wa 2009-10,akafunga bao katika mechi yao dhidi ya Barnet iliyoisha 2-2.Ilichezwa Underhill 19 Julai 2009. Barazite alishiriki katika ushindi wa Arsenal wa 2-0 dhidi ya West Brom katika Shindano la Kombe la Carling alipoingia na kumtoa Armand Traore baada ya dakika 69.

Wasifu wa Kimataifa

hariri

Barazite alichezea timu ya Uholanzi ya vijana walio chini ya umri wa miaka 17,akawa katika timu ya UEFA ya Uropa ya 2007 ya shindano hilo.Alifunga bao katika mechi ya Uholanzi na Ubelgiji iliyoisha 2-2.Uholanzi haikupita mkondo wa vikundi. Alikuwa mchezaji wa mara kwa mara katika timu yao ya vijana walio chini ya umri wa miaka katika mechi ya kuhitimu kucheza katika Shindano la Mabingwa la Uropa la 2009.Walikosa kuhitimu kuingia shindano hilo. Tarehe 9 Oktoba, yeye alicheza katika mechi ya kuhitimu kuingia Shindano la Mabingwa la Uropa,akawa mchezaji mbadala katika nusu ya pili.

Takwimu ya Wasifu

hariri
Klabu Msimu Ligi Kombe la FA Kombe la Carling Kombe la Uropa Jumal
Mechi alizocheza Mabao Mechi alizocheza Mabao Mechi alizocheza Mabao Mechi alizocheza Mabao Mechi alizocheza Mabao
Arsenal 2007–08 0 0 0 0 2 0 0 0 2 0
Derby County 2008–09 30 1 4 0 2 0 0 0 36 1
Arsenal 2009–10 0 0 0 0 1 0 0 0 1 0

Viungo vya nje

hariri
  1. "Nacer Barazite". Arsenal.com. Ilihifadhiwa 10 Januari 2011 kwenye Wayback Machine.
  2. BBC Sport. "Sheffield United 0-3 Arsenal".
  3. BBC Sport. "Blackburn 2-3 Arsenal (aet)"
  4. therams.co.uk. Nacer iakiwa Derby Ilihifadhiwa 11 Februari 2009 kwenye Wayback Machine.
  5. "Derby 4-1 Blackpool". BBC.. [1].
  6. uefa.com.. UEFA.
  7. uefa.com. Michuano ya shindano la mabingwala Uropa.

Viungo vya nje

hariri