Armand Traore

Mchezaji mprira wa Ufaransa

Armand Traoré (alizaliwa Paris, 8 Oktoba 1989) ni mchezaji wa mpira wa Ufaransa mwenye asili ya Senegal ambaye hivi sasa anacheza kama mchezaji wa kushoto na nyuma katika timu ya Arsenal.

Armand Traoré
Maelezo binafsi
Jina kamili Armand Traoré
Tarehe ya kuzaliwa 8 Oktoba 1989
Mahala pa kuzaliwa    Paris, Ufaransa
Maelezo ya klabu
Klabu ya sasa Arsenal
Namba 30
Klabu za vijana
Monaco Arsenal
Klabu za ukubwani
Miaka Klabu
Portsmouth katika mpango wa mkopo
Timu ya taifa
Ufaransa

* Magoli alioshinda

Wasifu wa Klabu

hariri

Arsenal

hariri

Traoré alijiunga na Arsenal mnamo tarehe 1 Agosti 2006, akiwa hapo awali ametoka timu ya AS Monaco. Ingawa,yeye hucheza katika timu hifadhi ya Arsenal,amecheza mechi 6 kama mmoja wa ligi ya FA ya timu hifadhi katika msimu wa 2005-2006,alicheza pia katika mechi ya makumbusho ya Dennis Bergkamp dhidi ya Ajax hapo Julai 2006. Alikuwa katika kikosi sha wachezaji 18 waliochaguliwa kucheza dhidi ya Dinamo Zagreb katika mechi ya Ligi ya Mabingwa-ingawa hakucheza.

Msimu wa 2006/07

hariri

Traoré alichezea timu rasmi ya Arsenal katika mchuano wao katika Shindano la Kombe la Carling dhidi ya West Bromwich Albion mnamo 24 Oktoba 2006, akichukua nafasi ya Emmanuel Adebayor aliyetolewa. Yeye aliendelea na kuanza katika mechi za Arsenal katika Shindano la Kombe la League dhidi ya Everton,Liverpool,mikondo yote miwili ya semi fainali dhidi ya Tottenham Hotspur na fainali dhidi ya Chelsea,Arsenal ilishindwa 2-1.

Msimu wa 2007/08

hariri

Katika mwezi wa Septemba, Traoré alirudi uwanja wa White Hart Lane, lakini wakati huu akiwa shabiki tu baada ya kushikwa akibeba nguo haramu akiingia uwanja huo. Yeye pia alicheza katika mechi dhidi ya Burnley ,lakini alitolewa na Justin Hoyte kuingia katika dakika ya 71. Alikuwa katika timu(ingawa hakucheza) katika mechi ya ushindi wa 3-1 dhidi ya Manchester City tarehe 2 Februari 2008. Yeye hatimaye alipata nafasi ya kucheza katika ligi kuu kwa mara ya kwanza katika mechi dhidi ya Liverpool,tarehe 5 Aprili 2008. Yeye alikuwa akitumika kama mchezaji katika ubawa wa kushoto katika mechi mbili za mwisho za ligi za Arsenal(msimu wa 2007-2008) huku akimpa pasi nzuri sana Nicklas Bendtner ndipo Nicklas akafunga dhidi ya Everton. Tarehe 4 Agosti 2008, alitia saini mkataba wa muda mrefu na Arsenal.

 
Armand akionyesha umahiri wake katika mechi

Msimu wa 2008/09

hariri

Tarehe 21 Agosti 2008, Traoré alitia saini mkataba wa mkopo wa urefu wa msimu mmoja katika klabu ya Portsmouth ili aweze kupata uzoefu wa kucheza katika ligi kuu. Traoré alifunga bao yake ya kwanza ya ligi kuu tarehe 18 Mei 2009 katika mechi ya nyumbani dhidi ya Sunderland. Portsmouth ilienda na kushinda mechi hiyo 3-1.

Msimu wa 2009/10

hariri

Armand Traore alirudi Arsenal na alihusika katika ushindi wa 2-0 wa Arsenal dhidi ya West Bromwich katika shindano la Kombe la Carling, alicheza kwa dakika 69 kabla ya kutolewa na Nacer Barazite kuingia. Gael Clichy na Kieran Gibbs walipopata majeraha , Traore alipata nafasi ya kucheza katika timu ya kwanza ya klabu. Yeye alianza kucheza mechi yake ya ligi dhidi ya Sunderland. Traore,mwenyewe alijeruhiwa, na akakosa mechi kadhaa lakini akarudi katika ushindi dhidi ya Aston Villa wa 3-0.

Wasifu wa Kimataifa

hariri

Armand huchezea timu ya taifa ya Ufaransa ya wachezaji chini ya umri wa miaka 19. Yeye aliwasaidia kuhitimu raundi ya Elite katika Shindano la UEFA la Vijana chini ya umri wa miaka 19 la 2008. Yeye alishiriki katika mechi zote 3 na moja ya raundi ya Elite kabla ya kushindwa na kutolewa kwenye shindano na timu ya Uitalia.

Alichaguliwa kama mmoja wa timu ya wachezaji chini ya umri wa miaka 21 kwa mara ya kwanza hapo 13 Novemba katika mechi yao na Denmark. Matokeo ya mechi yalikuwa ushindi wa 1-0 huku Traore akicheza dakika 73 kabla ya kubadilishwa na mchezaji mwingine.

Takwimu ya Wasifu

hariri
Klabu Msimu Ligi Kombe la FA Kombe la League Uropa Total
Mechi aliyocheza Mabao Pasi zilizosababisha bao Mechi aliyocheza Mabao Pasi zilizosababisha bao Mechi aliyocheza Mabao Pasi zilizosababisha bao Mechi aliyocheza Mabao Pasi zilizosababisha bao Mechi aliyocheza Mabao Pasi zilizosababisha bao
Arsenal 2006–07 0 0 0 1 0 0 6 0 0 0 0 0 7 0 0
2007–08 3 0 1 2 0 0 4 0 1 2 0 0 11 0 2
Portsmouth (mpango wa mkopo) 2008–09 19 1 0 2 0 0 1 0 0 6 0 0 28 1 0
Arsenal 2009-10 7 0 0 0 0 0 2 0 0 0 0 0 9 0 0
Kwa Jumla 29 1 1 5 0 0 12 0 1 9 0 0 55 1 2

Marejeo

hariri
  1. "Aliadière asaidia Arsenal". The Independent. 2006-10-25. http://sport.independent.co.uk/football/news/article1927194.ece Ilihifadhiwa 6 Novemba 2006 kwenye Wayback Machine..
  2. [1] Ilihifadhiwa 8 Februari 2009 kwenye Wayback Machine.
  3. [2]

Viungo vya nje

hariri