Nadharia ya uhusianifu
Nadharia ya uhusianifu iliundwa na Albert Einstein na inajumlisha nadharia ya uhusianifu maalumu (mwaka 1905) na nadharia ya uhusianifu ya jumla (1916).
Uhusianifu maalumu husema:
- Kasi ya nuru huwa sawa kwa wachunguzi wote wenye kasi isiyobadilika.
Uhusianifu wa jumla huelezea mvutano kama mviringo wa nafasiwakati. Huendeleza nadharia ya uvutano ya Isaac Newton. Hutumiwa na fizikia ya ulimwengu ya kisasa.
Majaribio mengi yamethibitisha nadharia zote mbili,[1] kama vile majaribio ya Michelson-Morley na majaribio ya Ives-Stilwell (uhusianifu maalumu), na majaribio wa Pound-Rebka (uhusianifu wa jumla).
Marejeo
haririMakala hii kuhusu mambo ya fizikia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Nadharia ya uhusianifu kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |