Natal ilikuwa koloni ya Uingereza katika Afrika ya Kuini-Mashariki tangu 1856. 1910 ikaingia kama jimbo la Natal katika Muungano wa Afrika Kusini pamoja na koloni nyingine za Rasi, Transvaal na Dola Huru.

Ramani inaonyesha eneo la jimbo la Natal (na. 4, rangi nyekundu-nyeupe) pamoja na maeneo ya KwaZulu (njano) ndani ya Afrika Kusini kabla ya 1994

1994 jimbo la Natal liliunganishwa na bantustan ya KwaZulu kuwa jimbo jipya la KwaZulu-Natal.

Historia ya awali

hariri

Jina la Natal limetokana na mpelelezi na mbaharia Mreno Vasco da Gama aliyefika kwenye pwani karibu na Durban mnamo 25 Desemba 1497. Aliita mahali Rio de Natal au "mto wa Krismasi" kutokana na tarehe ya kufika kwake. Jina limebaki kwenye ramani likaendelea kutumiwa kwa eneo hili.

Mwaka 1824 mfalme Shaka Zulu alikutana hapa na kikosi cha Waingereza akawa rafiki wa afisa kiongozi akampa zawadi ya kanda la eneo lenye urefu wa maili 25 kwenye pwani na upana wa maili 100 kuingia barani. Waingereza hawakujaribu kutawala eneo hili lote lakini walianzisha makazi ya Port Natal yaliyokuwa baadaye mji wa Durban.

1839 kundi la makaburu aina ya voortrekker lilifika Natal na kuanzisha mji wa Pietermaritzburg iliyokuwa mji mkuu wa jamhuri ndogo ya Natalia.

Baada ya miaka mitatu Waingereza kutoka rasi 1842 walitwaa jamhuri ya makaburu kwa nguvu ya kijeshi na kuiunganisha na koloni ya rasi. Makaburu wengi waliondoka kwenda eneo ng'ambo ya mto Oranje walipoanzisha Dola Huru ya Oranje.

Natal ilitawaliwa kwa muda kama sehemu ya rasi lakini ikapewa cheo cha koloni ya pekee kuanzia 1856.

Natal ni eneo la Zulu hasa. Kuna kundi kubwa ya watu wenye asili ya Uhindi waliopelekwa hapa na Waingereza kama wafanyakazi kwenye mashamba ya miwa na katika migodi wakati wa karne ya 19. Makaburu walibaki wachache tu na Watu wenye asili ya Kiingereza waliingia hapa kutoka rasi.

  Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika Kusini bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Natal kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.