Wazulu
(Elekezwa kutoka Zulu)
Wazulu (kwa Kizulu: amaZulu) ni kabila kubwa la Afrika Kusini lenye watu milioni 9-10. Makazi yao ni hasa jimbo la KwaZulu-Natal lakini wako katika miji yote ya Afrika Kusini pamoja na vikundi vidogo zaidi katika Zimbabwe, Zambia na Msumbiji.
Lugha yao ya Kizulu, wanayoita wenyewe "isiZulu", ni ya Kibantu.
Katika historia ya Afrika Kusini ufalme wa Wazulu na upanuzi wake chini ya Shaka Zulu ni kipindi muhimu. Dola la Wazulu likatetea uhuru wake hadi mwaka 1879 liliposhindwa na Waingereza.
Wakati wa siasa ya apartheid Wazulu kama Waafrika wote walihesabiwa kama raia wa ngazi duni.
Tangu mwisho wa apartheid hushiriki kikamilifu katika ujenzi wa taifa.
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Wazulu kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |